Ezra alikuwa ameuelekeza moyo wake kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda.
Ezra 7:10.
Akiwa amezaliwa kutoka kwa wana wa Haruni, Ezra alikuwa amepewa mafunzo ya kikuhani; na zaidi ya hilo alikuwa amepata ufahamu wa maandishi ya waganga, wanajimu na wenye hekima wa dola ya Wamedi na Waajemi. Lakini hakuridhishwa na hali yake ya kiroho. Alitamani kuwa katika upatanifu kamili na Mungu; alitamani hekima ili kutenda mapenzi ya Mungu…. Hii ilimfanya ajiingize kwa bidii katika majifunzo ya historia ya watu wa Mungu, kama yalivyorekodiwa kwenye maandiko ya manabii na wafalme. Alichunguza vitabu vya kihistoria na vya kinabii vya Biblia ili ajue kwa nini Bwana alikuwa ameruhusu Yerusalemu iangamizwe na watu wake wachukuliwe mateka hadi kwenye nchi ya kipagani…
Alijifunza juu ya maelekezo yaliyotolewa kwenye Mlima Sinai na katika kipindi kirefu cha kutangatanga jangwani. Kadiri alivyozidi kujifunza zaidi na hata zaidi kuhusu namna Mungu anavyoshughulika na watoto wake, na kuelewa utakatifu wa sheria iliyotolewa pale Sinai, moyo wa Ezra uliamshwa. Alipata uongofu mpya tena wa kina na akakusudia kujua vizuri taarifa za historia takatifu, ili atumie ujuzi huu kuleta baraka na nuru kwa watu wake.
Ezra alijitahidi kuandaa moyo kwa ajili ya kazi ambayo aliamini ilikuwa mbele yake. Alimtafuta Mungu kwa bidii, ili apate kuwa mwalimu mwenye hekima katika Israeli. Alipoendelea kusalimisha akili na nia yake kwa udhibiti wa Mungu, aliletewa maishani mwake kanuni za utakaso wa kweli, ambao, miaka ya baadaye, zilikuwa na mguso unaotengeneza, sio tu kwa vijana waliohitaji maelekezo, bali pia kwa wengine wote waliohusiana na Mungu…
Ezra akawa msemaji wa Mungu, akiwaelimisha wale waliokuwa naye kanuni zinazotawala mbinguni… Iwe ni karibu na ikulu ya mfalme wa Wamedi na Waajemi au kule Yerusalemu, kazi yake ya msingi ilikuwa ualimu. Kadiri alivyoendelea kuwasiliana na wengine juu ya ukweli aliokuwa amejifunza, ndivyo uwezo wake wa utendaji ulivyoongezeka. Akawa mtu wa utauwa na ari. Akawa shahidi wa Bwana kwa ulimwengu kuhusu nguvu ya ukweli wa Biblia uwezavyo kufanya maisha ya kila siku yawe ya kiungwana.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon