Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.
Ufunuo 22:11.
Inapasa wale wote ambao wanataka majina yao yabaki kwenye kitabu cha uzima, sasa, katika siku chache zilizobaki za rehema, watese nafsi zao mbele za Mungu kwa kuhuzunikia dhambi na kwa toba ya kweli. Ni lazima pawepo na kujichunguza nafsi kwa kina, kwa uaminifu. Roho ya kutokuwa makini, ya kupenda upuuzi ambayo imeendekezwa na wengi wanaojiita Wakristo ni lazima itupiliwe mbali. Lipo pambano zito mbele za wote watakaoshinda uelekeo wa uovu ambao unajitahidi kuwatawala. Kazi ya maandalizi ni kazi ya mtu mmoja mmoja. Hatuokolewi kwa makundi. Usafi na kujitoa kwa mtu mmoja hakutafidia hitaji la mwingine kwa ajili ya sifa hizi….Lazima kila mmoja ajaribiwe na akutwe akiwa bila doa wala kunyanzi wala chochote kama hicho.
Matukio yenye muunganiko na kufungwa kwa kazi ya upatanisho ni mazito. Vyote vinavyohusika na matukio haya ni vya maana sana. Hukumu inafanyika sasa kwenye hekalu mbinguni… Maisha yetu yapasa yapitiwe mbele za utisho wa kuwepo kwake Mungu…
Kazi ya hukumu ya upelelezi itakapofungwa, hatima ya wote itakuwa imeamuliwa kwa ajili ya uzima au mauti. Rehema itakuwa imefikia mwisho muda mfupi kabla ya kutokea kwa Bwana mawinguni mbinguni… Wale ambao wanapochoka kukesha, wanageukia mivuto ya dunia wamo katika hali ya hatari sana. Wakati mtu wa biashara anapojikita kwenye utafutaji wa faida, wakati mpenda anasa anapozitafuta anasa, wakati binti wa mitindo anapopanga mapambo yake, -- inaweza kuwa katika saa hiyo Hakimu wa dunia yote atatoa kauli, “Umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.”
Kwa utulivu, bila kutambulika kama alivyo mwizi usiku wa manane, ile saa ya kilele cha uamuzi ambayo itakuwa ni ishara ya hitimisho la hatima ya kila mtu, kuondolewa kwa mwisho kwa rehema ambayo imekuwa huru kwa wenye hatia. “Kesheni basi, … asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.”

EmoticonEmoticon