Ezra…alikuwa mwandishi mwepesi katika sheria ya Musa, aliyokuwa ameitoa Bwana, Mungu wa Israeli. Ezra 7:6.
Japo zaidi ya miaka elfu mbili imepita tangu Ezra alipouelekeza “moyo wake kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda,” kupita kwa muda hakujapunguza mguso wa kielelezo chake cha utauwa. Katika karne zote, rekodi ya maisha yake ya kujitoa wakfu imewatia moyo wengi kwa dhamira hii ya “kuitafuta sheria ya Bwana, na kuitenda.”
Makusudi ya Ezra yalikuwa ya juu na matakatifu; katika yote aliyoyafanya alisukumwa na upendo wa dhati kwa ajili ya roho za watu. Huruma na wema alivyovionesha kwa wale waliokuwa wametenda dhambi, iwe ni kwa kukusudia au kwa kutokujua, yapasa liwe ni jambo la kuangalia kwa wale wote wanaohitaji kuleta matengenezo….
Hakuna kitu kama kudhoofisha au kuimarisha sheria ya Yehova. Kama ambavyo imekuwa, ndivyo ilivyo. Daima imekuwa hivyo na itakuwa hivyo daima, takatifu, yenye haki na njema, ikiwa kamili katika yenyewe. Haiwezi kutanguliwa wala kubadilishwa. “Kuiheshimu” au “Kutoiheshimu” ni hotuba ya watu…
Yapasa Wakristo wajiandae kwa ajili ya kile kitakachotokea duniani kama jambo la kushtua sana na inapasa wafanye maandalizi haya kwa kusoma neno la Mungu kwa bidii na kujitahidi kupatanisha maisha yao na kanuni zake. Masuala makuu ya milele yanatuhitaji tufanye kitu tofauti na dini ya kufikirika tu, dini ya maneno na mitindo, ambapo ile kweli inawekwa nje….
Kama watakatifu wa Agano la Kale walichukua ushuhuda wa utii uliong’aa kiasi hicho, je, haipasi wale ambao mkusanyiko wa nuru ya karne nyingi unawaangazia wachukue ushuhuda mkubwa zaidi unaodhihirisha nguvu ya ile kweli
Je, tutaruhusu mfano wa Ezra utufundishe namna ya kutumia ujuzi wa Maandiko?
Je, tutaruhusu mfano wa Ezra utufundishe namna ya kutumia ujuzi wa Maandiko?
Maisha ya mtumishi wa Mungu yapasa yawe msukumo kwetu kumtumikia Bwana kwa moyo na akili na nguvu. Kila mmoja wetu anayo kazi ya kufanya na hii inaweza kukamilishwa kwa jitihada iliyowekwa wakfu. Kwanza tunahitajika kujiweka katika hali ya kujua masharti ya Mungu na kisha kuyafanyia kazi. Ndipo tutaweza kupanda mbegu za ile kweli ambazo zitazaa matunda hadi uzima wa milele.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon