Ujiweke tayari kuonana na Mungu wako, Ee Israeli. Amosi 4:12, sehemu ya mwisho.
Maishani mwake jangwani, Yohana Mbatizaji alifundishwa na Mungu. Alijifunza udhihirisho wa Mungu katika viumbe vya asili. Chini ya uongozi wa Roho wa Mungu, alijifunza magombo ya manabii. Mchana na usiku, Kristo alikuwa ndilo somo lake, tafakuri yake, hadi akili na moyo na nafsi vilipojazwa kwa njozi ya utukufu. Alimtazama Mfalme katika uzuri wake akawa haioni nafsi yake. Aliona uzuri wa utakatifu akajua kutokuwa na ufanisi na kutokustahili kwake. Ni ujumbe wa Mungu ambao alipaswa kuutangaza. Alikuwa asimame kwa uwezo wa Mungu na haki yake. Alikuwa tayari kwenda mbele kama mjumbe wa mbinguni, bila kutishwa na watu, kwani aliviangalia vya Kimbingu….
Yohana alitangaza ujumbe wake bila hoja zilizofafanuliwa kwa undani zaidi au nadharia zilizotengenezwa vizuri. Kwa kushtusha na uthabiti, huku ikiwa imejawa tumaini, sauti yake ilisikika kutoka nyikani, “Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”… Wakulima na wavuvi ambao hawakuwa wameelimika kutoka kwenye nchi jirani; askari wa Kirumi kutoka kwenye makambi ya jeshi ya Herode; watawala wakiwa na majambia ubavuni mwao, wakiwa tayari kuangusha chochote ambacho kingeleta muonjo wa uasi; wakusanya kodi wenye uchu wa mali wakitokea kwenye vibanda vyao vya kukusanya kodi na kutoka Sanhedrin, makuhani waliokuwa wamebeba maandiko, -- wote walisikia kama waliopigwa na butwaa; nao wote … wakaenda…wakiwa wamechomwa mioyoni kwa kuzihisi dhambi zao…
Katika kipindi hiki, kabla tu ya kuja kwa mara ya pili kwa Kristo kwenye mawingu ya mbinguni, kazi kama ile ya Yohana sharti ifanywe. Mungu anaita watu watakaoandaa watu kusimama katika siku ile kuu ya Bwana… Tukiwa watu tunaoamini katika kuja upesi kwa Kristo, tunao ujumbe wa kupeleka,-- “ujiweke tayari kuonana na Mungu wako.” Sharti ujumbe wetu uwe wa kweli kama ulivyokuwa ujumbe wa Yohana. Alikemea wafalme kwa uovu wao. Bila kujali kwamba maisha yake yalikuwa hatarini, hakusita kutangaza neno la Mungu. Na kazi yetu katika kizazi hiki lazima ifanyike kwa uaminifu.
Ili tuweze kutoa ujumbe kama ule ambao Yohana aliutoa, ni lazima tuwe na uzoefu wa kiroho kama wake. Kazi ile ile sharti ifanywe ndani yetu. Ni lazima tumuone Mungu na katika kumwona Yeye, tusiendelee kuiona nafsi.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon