JAMBO LA PEKEE SANA KWANGU.



Tarehe na siku kama ya leo mama yangu mzazi baada ya miezi 9 ya maangaiko ndipo Mungu aliruhusu nami niwepo duniani.

Baba yangu na mama yangu mpenzi napenda kuwashukuru sana kwa upendo wenu kwangu na malezi mema juu yangu, mlinifundisha kumtegemea Mungu katika kila jambo ninayaona matunda mema mliyonifundisha tangu utoto wangu hata sasa ni mtu mzima sijaiacha njia mliyonilelela mbarikiwe sana!!!!

"Mlee mtoto katika njia impasayo,
Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Mithali 22:6.

Kubwa zaidi napenda kumshukuru Mungu wangu kwa ulinzi wake mkubwa KWANGU, ni hatari nyingi ikiwepo mishale ya mwovu amenivusha na kuniepusha nayo hata maadui zangu wamebaki kushangaa,.... Maana Mungu amekuwa ngome imara kwangu,
Pamoja na udhaifu na makosa yangu, Mungu wangu haukuniacha Wewe ni Baba unipendaye na kunijali, nitakupenda daima na kulitukuza jina lako mbele za watu milele zote.

"Jina la BWANA ni ngome imara;
Mwenye haki huikimbilia, akawa salama. Mithali 18:10"

Pia napenda kuwashukuru marafiki zangu, ndugu zangu na jamaa zangu kwa upendo wenu, ushauri na wema wenu kwangu, ni jambo la pekee kuwa pamoja katika hali zote ndivyo Mungu apendavyo.. "Upendano wa undugu na hudumu"

"Tazama, jinsi ilivyo vema, na kupendeza,
Ndugu wakae pamoja, kwa umoja. Zaburi 133:1"

Mungu awabariki sana ndugu zangu, marafiki zangu, na jamaa zangu wote na maadui zangu, palipo na makosa tusamehane na tuvumiliane sisi wote ni wadhaifu tupendane na kuchukuliana mizigo kwa upole na upendo, pia Mungu awabariki ili upendo utawale na chuki iondoke, Mungu awe kiini cha mawazo yetu daima siku zote.

Kikubwa zaidi tukaze mwendo tusimame kiume, ushindi uko mbele yetu,.... Kristo yuko mlangoni tumeandaliwa taji tutakaposhinda.
Mungu awabariki sana.
Image may contain: 1 person, smiling, standing
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.