PATAKATIFU NI NINI?!



Sehemu ya......... 2.

Lakini Mungu alikuwa ameongoza watu wake katika vuguvugu kuu la marejeo; nguvu na utukufu wake vilitenda kazi, na hivyo asingeruhusu viishie gizani na kukatishwa tamaa, kushutumiwa kuwa uongo na msisimko wa kishupavu. Asingeacha neno lake litiliwe mashaka na lisiaminike. 
Ingawa wengi walijitenga na uzingatiaji wao wa awali wa vipindi vya unabii na kukataa usahihi wa harakati za vuguvugu zilizojengwa juu yake, wengine hawakutaka kupinga vipengele vya imani na uzoefu uliojengeka kutokana na Maandiko na ushahidi wa Roho wa Mungu. Waliamini kwamba walikuwa wameshika na kutumia kanuni kuu za kutafsiri katika kujifunza kwao unabii, na kwamba ulikuwa wajibu wao kushikilia imara kweli walizokwisha zipata tayari, na kuendeleza kazi hiyo ya uchunguzi wa Biblia. Kwa maombi ya juhudi walipata upya msimamo wao na kusoma Maandiko ili kugundua kosa lao. Waliposhindwa kuona kosa lo lote katika kuhesabu kwao vipindi vya unabii, waliongozwa kuchunguza kwa makini kabisa somo la patakatifu.

Katika uchunguzi wao walijifunza kwamba kulikuwa hakuna ushahidi wo wote wa Maandiko unaokubaliana na mtazamo uliopendwa sana na kuaminiwa na watu wengi kwamba dunia ndio patakatifu; bali walikuta Biblia imejaa ufafanuzi juu ya somo la Patakatifu, chanzo chake, mahali pake maalumu, na huduma zake; shuhuda za waandishi watakatifu zikiwa wazi sana na za kutosha kulifanya lisiwepo swali juu yake. Mtume Paulo katika waraka wake kwa Waebrania, anasema: Basi hata agano la kwanza lilikuwa pia na kawaida za huduma takatifu, na Patakatifu pa kidunia. Maana hema lilitengenezwa; la kwanza mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate ya wonyesho; ndipo palipoitwa patakatifu. Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa Patakatifu, yenye chetezo cha dhahabu, na sanduku la agano lililofunikwa kwa dhahabu pande zote, mlimokuwa na kopo la dhahabu lenye ile mana, na fimbo ya Haruni iliyochipuka, na vile vibao vya agano; na juu yake makerubi ya utukufu, yakitia kivuli kiti cha Rehema."
Waebrania 9:1-5.(KJV).

Patakatifu anapopanukuu Paulo hapa palikuwa ni hema lililojengwa na Musa kwa agizo la Mungu kama mahali pa kidunia pa Mungu kukaa.
"Nao wanifanyie Patakatifu; ili nipate kukaa kati yao" (Kutoka 25:8), lilikuwa agizo alilopewa Musa wakati akiwa pamoja na Mungu mlimani. Waisraeli walikuwa wakisafiri kupitia jangwani, kwa hiyo hema lilijengwa kwa namna ambayo lingeweza kuhamishwa kutoka mahali hadi mahali; hata hivyo lilikuwa jengo lenye utukufu Mkuu. Kuta zake zilisimamishwa wima kwa mbao nzito zilizo funikwa kwa dhahabu safi na ndani kuliwekwa soketi za fedha, wakati paa liliundwa kwa mapazia ya aina mbalimbali, au mifuniko, sehemu ya nje kwa ngozi, Patakatifu mno kwa kitani safi na kupendezwa kwa maumbo ya makerubi. Kando ya ua wa nje ambao ulikuwa madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, hema lenyewe lilikuwa na vyumba viwili vilivyoitwa Patakatifu na Patakatifu mno vilivyotenganishwa kwa pazia la gharama kubwa na la kifahari; au pazia la kawaida; pazia kama hilo lilifunika sehemu ya sehemu ya kuingilia kwenye chumba cha kwanza.

Inaendelea tafadhari baki nasi......

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.