Sehemu ya............. 3.
Ndani ya Patakatifu kulikuwa na kinara cha taa, upande wa kusini, kikiwa na taa zake saba zikitoa nuru kwenye hekalu wakati wote mchana na usiku; upande wa kasikazini kulisimama meza ya mikate ya wonyesho; na mbele ya pazia lililotenganisha patakatifu na patakatifu mno kulikuwa na madhabahu ya kufukiza uvumba, ambayo kutoka juu yake wingu la harufu nzuri, pamoja na maombi ya Israeli, kila siku yalikuwa yanapaa mbele za Mungu.
Ndani ya patakatifu mno kulisimama sanduku, sanduku la mbao za thamani kubwa lililonakishiwa kwa dhahabu, ghala la mbao mbili za mawe ambazo juu yake Mungu alikuwa ameandika sheria ya Amri kumi.
Juu ya sanduku, na kifuniko kilichofunika sanduku takatifu, kulikuwa na kiti cha rehema, chenye utukufu kilichotengenezwa kwa ustadi mkubwa, kikiwa kimefunikwa juu yake na makerubi wawili, mmoja kila upende, na wote wakiwa wamefuliwa kwa dhahabu safi. Katika chumba hiki uwepo wa Mungu ulidhihirishwa katika wingu la utukufu katikati ya makerubi.
Baada ya Waebrania kukaa Kanaani, hema takatifu lilibadilishwa kwa hekalu la Sulemani. (nafasi ya hema takatifu ilichukuliwa na hekalu la Sulemani), ambalo, ingawa lilikuwa jengo la kudumu na kubwa lilifanyakazi zile zile na lilikuwa na mfano ule ule. Hema takatifu liliendelea katika muundo huu isipokuwa lilipobomolewa katika maangamizo katika wakati wa Danieli - mpaka maangamizo yake na Warumi katika mwaka wa 70 BK.
Hili ndilo hema takatifu pekee kuwahi kuwepo duniani, ambalo Biblia hueleza habari zake. Hili lilielezwa na Paulo kuwa hema takatifu la Agano la kwanza. Lakini Je, agano jipya halina hema takatifu?!
Watafutaji wa ukweli wakirudia tena kwenye kitabu cha Waebrania, waliona kwamba kuwepo kwa hema takatifu la pili au hema takatifu la agano jipya kumeonyeshwa katika maneno ya Paulo ambayo tayari yamekwisha kunukuliwa hapo nyuma: "Basi hata agano la kwanza lilikuwa pia na kawaida za huduma takatifu, na patakatifu pa dunia." Utumiaji wa neno "pia" huonyesha kuwa Paulo hapo awali alikuwa ameeleza kuhusu hema takatifu hili. Wakirudi nyuma, mwanzoni mwa sura iliyotangulia, walisema: "Basi katika hayo tunayosema, neno lililo kuu ndilo hili: Tunaye Kuhani Mkuu wa namna hii, aliyewekwa mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha ukuu mbinguni; mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu." Waebrania 8:1-2(KJV).
Hapa pamefunuliwa hema takatifu la agano jipya. Hema takatifu la kwanza liliwekwa na mwanadamu, lilijengwa na Musa; lakini hili linawekwa na Bwana, siyo Mwanadamu. Katika hili la pili, Kristo, Kuhani wetu Mkuu, uhudumu akiwa upande wa mkono wa kuume wa Mungu.
Hema takatifu moja lilikuwa duniani, na lingine liko mbinguni.
Itaendelea tafadhari baki nasi.......
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon