Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Warumi 12:1.
Bwana amekuwa akiita watu wake wawe macho na matengenezo ya afya. Hii ni moja ya matawi makuu ya kazi ya maandalizi ya kuja kwa Mwana wa mtu. Yohana Mbatizaji alienda katika roho na nguvu ya Eliya kuandaa njia ya Bwana….
Yohana alijitenga na marafiki na starehe za maisha. Usahili wake katika kuvaa, vazi lililofunwa kwa ngozi ya ngamia, lilikuwa kemeo lililokuwa dhahiri dhidi ya ubadhirifu na hali ya kujionesha kwa makuhani wa Kiyahudi na ya watu kwa ujumla. Lishe yake, ya mboga kabisa, ya nzige na asali mwitu, ilikuwa kemeo dhidi ya hali ya uendekezaji wa uchu wa kula na ulafi vilivyokuwa vimetawala kila mahali… Wale inaowapasa waandae njia kwa ajili ya kuja kwa Kristo mara ya pili wanawakilishwa na Eliya mwaminifu, kama ambavyo Yohana alikuja kwa roho ya Eliya ili kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa mara ya kwanza wa Kristo. Somo kuu la matengenezo sharti lihamasishwe…. Yapasa kiasi katika mambo yote liwe jambo linalounganishwa na ujumbe, kugeuza watu wa Mungu watoke katika ibada ya sanamu, ulafi wao na ubadhirifu wao katika mavazi na mambo mengine.
Hali ya kujikana nafsi, unyenyekevu na kiasi ambavyo vinahitajika kwa mwenye haki, ambaye Mungu anamwongoza kwa namna ya pekee na kumbariki, sharti viwasilishwe kwa watu dhidi ya mazoea ya ubadhirifu, yanayoharibu afya ya wale wanaoishi kwenye kizazi hiki kilichoharibika… Hakuna sababu nyingine kubwa zaidi inayosababisha uharibifu kimwili na kimaadili kama ilivyo kupuuzia somo hili muhimu. Wale wanaoendekeza uchu na hisia zao, huku wakifumba macho yao dhidi ya nuru wakihofu kuwa wataona tabia za uovu ambazo hawapo tayari kuziacha, wanayo hatia mbele za Mungu. Yeyote ageukaye anayeipa nuru mgongo katika suala moja hufanya moyo wake kuwa mgumu kiasi cha kutojali nuru katika mambo mengine. Yeyote anayekiuka majukumu ya kimaadili katika maeneo ya kula na kuvaa huwa anaandaa njia ya kukiuka madai ya Mungu yanayohusiana na masuala ya milele. Miili yetu si mali yetu wenyewe. Mungu anayo madai kwetu ya kuwa waangalifu juu ya mazingira ambayo ametupatia, ili tupate kuwasilisha miili yetu kwake kama dhabihu iliyo hai, takatifu na ya kumpendeza.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon