PATAKATIFU NI NINI?!



Sehemu ya....... 4.

Pia, hema lililojengwa na Musa lilifanywa kama kielelezo. Bwana alimwamuru: "Sawasawa na haya yote nikuonyeshayo, kama mfano wa hema, na mfano wa vyombo vyake vyote, ndivyo mtakavyolifanya." Agizo lilitolewa tena, "Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, ulioonyeshwa mlimani. Kutoka 25:9,40. Paulo anasema kwamba hema la kwanza "kilikuwa mfano kwa ajili ya wakati huu uliopo sasa; wakati huo sadaka na dhabihu zilitolewa;" kwamba patakatifu pake palikuwa "mfano wa mambo ya mbinguni," kwamba makuhani walitoa dhabihu sawasawa na sheria iliyotumika "kwa mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni," na kwamba "Kristo hakuingia mahali Patakatifu palipotengenezwa kwa mikono, ambayo ndiyo mfano wa patakatifu halisi, lakini aliingia mbinguni kwenyewe, aonekane sasa usoni pa Mungu kwa ajili yetu." Waebrania 9:9,23; 8:5; 9:24.

Hema takatifu lililoko mbinguni, ambamo Yesu anahudumu kwa ajili yetu ndilo halisi kabisa, ya hema lililojengwa na Musa ambalo lilikuwa mfano. Mungu aliweka Roho wake juu ya wajenzi wa hema takatifu la duniani. Ufundi stadi iliotumika katika ujenzi wake ulikuwa udhihirisho wa hekima takatifu ya mbinguni. Kuta zilikuwa na mwonekano wa dhahabu kubwa na imara, ikiakisi nuru ya kinara cha taa saba za dhahabu kila upande. Zuria zuri sana lililounda dari, lililopambwa kwa urembo wa maumbo ya malaika kwa rangi ya bluu na zambarau na nyekundu, ziliongeza uzuri wa mandhari. Juu ya pazia la pili kulikuwa na shekina takatifu, mwonekano wa udhihirisho wa utukufu wa Mungu, ambao mtu mwingine yeyote isipokuwa Kuhani Mkuu asingeweza kupita mbele yake na kuishi.

Miale ya mng'ao wa fahari wa hema la duniani iliakisi mawazo ya mwanadamu utukufu wa hekalu la mbinguni ambako Kristo mtangulizi wetu anahudumu kwa ajili yetu mbele ya kiti cha enzi cha Mungu. Mahali akaapo Mfalme wa wafalme, ambapo elfu maelfu wanamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wanasimama mbele yake (Danieli 7:10); hekalu hilo lililojazwa kwa utukufu wa Ufalme wa milele, mahali ambapo maserafi, walinzi wake wanaong'aa, hufunika nyuso zao kwa kuabudu na kusujudu, wanapatikana ndani ya jengo lenye utukufu mwingi mno kuwahi kujengwa kwa mikono ya mwanadamu, na lisiloweza kuonekana vizuri kutokana na ukubwa na utukufu wake usio na kiwango. Bado kweli zake muhimu kuhusiana na hekalu la mbinguni na ukuu wa kazi inayoendelea kufanyika pale kwa ajili ya Ukombozi wa mwanadamu vilifundishwa kwa hema takatifu la duniani na huduma zake.

Sehemu takatifu za hekalu mbinguni zinawakilishwa na vyumba viwili ndani ya hema takatifu la duniani. Mtume Yohana alipewa mwonekano wa hema la Mungu mbinguni katika maono, aliona pale 'taa za moto zikiwaka mbele ya kiti cha enzi." Ufunuo 4:5, Alimwona malaika "akiwa na chetezo cha dhahabu; akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu iliyo mbele ya kiti cha enzi" Ufunuo 8:3 Hapa nabii aliruhusiwa kuona chumba cha kwanza cha hekalu la mbinguni; na akaona pale "taa saba za moto" na "Madhabahu ya dhahabu," vikiwakilishwa na kinara cha mshumaa wa dhahabu na madhabahu ya uvumba katika hema takatifu la duniani.
Tena "hekalu la Mungu likafunguliwa" Ufunuo 11:19 na akatazama ndani ya pazia, katika patakatifu pa patakatifu. Hapa aliona "sanduku la agano lake," likiwakilishwa na sanduku takatifu lililo tengenezwa na Musa kutunza amri za Mungu.

Hivyo ndivyo wale waliokuwa wakijifunza somo hili walivyopata ushahidi usiopingika wa kuwepo kwa hekalu mbinguni. Musa alifanya hema takatifu la duniani kutokana na kielelezo alichokuwa ameonyeshwa.
Paulo anafundisha kwamba kielelezo hicho kilikuwa ni hekalu halisi lililoko mbinguni. Na Yohana atathibitisha kuwa aliliona mbinguni.

Itaendelea tafadhari baki nasi...........

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: 2 people, people smiling, text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.