PATAKATIFU NI NINI?!



Sehemu ya........... 5

Katika hekalu mbinguni, mahali pa makao ya Mungu, utawala wake umejengwa katika haki na hukumu. Sheria yake, ambayo ni kiongozi Mkuu wa haki ambayo wanadamu wote wanapimwa kwako, iko Patakatifu pa Patakatifu. Sanduku linalotunza mbao mbili za amri linafunikwa na kiti cha rehema, ambapo Kristo anaombea wenye dhambi kwa damu yake. Hivyo ndivyo Muungano wa haki na rehema unavyowakilishwa katika mpango wa Ukombozi wa mwanadamu. Hekima ya Mungu peke yake ndio inayoweza kubuni Muungano huu na kukamilishwa kwa nguvu za Mungu; ni Muungano ambao huijaza mbingu yote kwa mshangao na ibada. Makerubi wa hema takatifu la Duniani, wakitazama chini kwa kicho juu ya kiti cha rehema, huwakilisha upendo ambao jeshi la mbinguni huzingatia, huinua na kutazamia kazi ya Ukombozi.

Hii ni siri ya rehema ambayo malaika hupenda kuitazama - kwamba Mungu anaweza kuwa mwenye haki wakati anapomhesabia haki mwenye dhambi atubuye na kufanya upya uhusiano wake na jamii ya wanadamu iliyoanguka; kwamba Kristo anaweza kujitweza kuinama kuinua umati wa watu usio na idadi kutoka katika lindi kuu la maangamizi na kuwavika kwa mavazi yasiyo na mawaaa ya haki yake mwenyewe kuwaunganisha pamoja na malaika ambao kamwe hawajawahi kuanguka na kukaa milele mbele za Mungu.

Kazi ya Kristo kama Mwombezi wa mwanadamu inaelezwa katika unabii huo mzuri wa Zekaria kuhusiana naye "ambaye jina lake ni Tawi."
Nabii anasema: "Yeye atalijenga hekalu la Bwana; naye atauchukua huo utukufu; ataketi na kutawala katika kiti chake (cha Babaye) cha enzi; naye atakuwa kuhani katika kiti chake (cha Babaye) cha enzi: na Shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili." Zekaria 6:12-13.

"Alijitenga hekalu la Bwana". Kwa njia ya kafara yake na upatanisho wake Kristo ni vyote viwili ni msingi na ni mjenzi wa kanisa la Mungu.
Mtume Paulo anaelekeza kwake kama "Jiwe kuu la pembeni katika Yeye jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana; katika yeye ninyi nanyi Anasema " mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho." Waefeso 2:20 - 22.

"Atachukua utukufu" Utukufu wa Ukombozi kwa ajili ya jamii ya wanadamu iliyoanguka uko kwa Kristo. Katika Vizazi vyote milele na milele, wimbo wa waliokombolewa utakuwa: "Kwake yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,.....utukufu na ukuu una yeye hata milele na milele." Ufunuo 1:5-6.

Itaendelea tafadhari baki nasi..........

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.