Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.
Yohana 3:29.
Yohana 3:29.
Katika kila hatua ya historia ya dunia hii, Mungu amekuwa na mawakala wake wanaoendeleza mbele kazi yake… Yohana Mbatizaji alikuwa na kazi maalumu, aliyozaliwa kwa ajili yake na ambayo aliteuliwa kwayo – kazi ya kuandaa njia ya Bwana.
Baada ya huduma ya Kristo kuanza, wakati wanafunzi wa Yohana walipomjia wakilalamika kwamba watu wote walikuwa wakimfuata Mwalimu mpya, Yohana alionesha wazi kwamba alielewa uhusiano wake na Masihi, alionesha pia jinsi alivyofurahi kumkaribisha Yule ambaye kwa ajili yake alikuwa ameiandaa njia.
Yohana alikuwa ameitwa kuongoza njia kama mwanamatengenezo. Kwa sababu ya hili, wanafunzi wake walikuwa kwenye hatari ya kukaza macho yao kwake… na kushindwa kuona ukweli kwamba yeye alikuwa chombo tu ambacho Mungu alikuwa amekifanya. Lakini kazi ya Yohana haikutosha kwa ajili ya kuweka msingi wa kanisa la Kikristo. Alipokamilisha utume wake, kazi nyingine ilipasa ifanyike, ambayo ushuhuda wake usingeikamilisha. Wanafunzi wake hawakuielewa hii. Walipomwona Kristo akiingia kuichukua kazi, wakawa na wivu na hali ya kutoridhika.
Hatari hiyo hiyo bado ipo. Huwa Mungu anamwita mtu ili afanye kazi fulani; na anapokuwa ameifanya hadi pale anapoweza kuifikisha, Bwana huleta wengine, ili waiendeleze zaidi. Lakini, kama wanafunzi wa Yohana, wengi huwa wanajisikia kwamba mafanikio ya kazi yanategemea yule mtendakazi wa kwanza. Mtazamo unawekwa kwa yule mwanadamu badala ya Mungu, wivu unaingia, nayo kazi ya Mungu inaharibika. Mtu ambaye ameheshimiwa kiasi kikubwa hivyo, huwa anajaribika kukuza hali ya kujiamini nafsi. Hatambui hitaji lake la kumtegemea Mungu. Watu wanafundishwa kumtegemea mwanadamu kwa ajili ya uongozi,…nao wanaongozwa mbali na Mungu.
Haikukusudiwa kwamba kazi ya Mungu ichukue sura na bango la mwanadamu. Wakati mmoja hadi mwingine, Bwana ataleta mawakala tofauti tofauti, ambao kupitia kwao makusudi yake yanaweza kutimizwa kwa namna iliyo bora zaidi. Wana heri wale ambao wako tayari kuacha nafsi inyenyekezwe, wakisema pamoja na Yohana Mbatizaji, “Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.”
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon