PATAKATIFU NI NINI?!



Sehemu ya............ 6

"Ataketi na kutawala katika kiti cha enzi." Sio sasa "Katika kiti cha enzi cha utukufu wake;" Ufalme wa utukufu bado haujaanzishwa. Ni mpaka kazi yake kama mpatanishi itakapokwisha ndipo Mungu "atampa kiti cha enzi cha Daudi" Ufalme ambao "hautakuwa na mwisho" Luka 1:32-33. Kama Kuhani, Kristo sasa anaketi na Baba katika kiti chake cha enzi. Ufunuo 3:21.
Katika kiti cha enzi pamoja na Mungu aishie milele, na aishie kwa nafsi yake mwenyewe kuna yeye ambaye "ameyachukua masikitiko yetu, na kujitwika huzuni zenu," ambaye "alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi." ili "aweze kuwasaidia wao wanaojaribiwa." "Kama mtu ye yote akitenda dhambi, tunaye Mwombezi kwa Baba." Isaya 53:4; Waebrania 4:15; 2:18; 1 Yohana 2:1. Uombezi wake ni ule wa mwili uliochomwa na kuharibiwa, wa maisha yasiyo na mawaa. Mikono iliyojeruhiwa, ubavu uliochomwa mkuki, miguu iliyoharibiwa, vinaomba kwa ajili ya mwanadamu aliyeanguka, ambaye Ukombozi wake ulinunuliwa kwa gharama hiyo isiyo na ukomo.

"Na Shauri la amani litakuwa kati ya hao wawili." Upendo wa Baba, ulio sawa na Upendo wa Mwana, ni chemchemi ya wokovu kwa ajili ya jamii ya mwanadamu iliyopotea. Yesu aliwaambia wanafunzi wake kabla hajaenda zake: "siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba: kwa maana Baba mwenyewe awapenda." Yohana 16:26-27.
Mungu alikuwa "ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake." 2 Wakorintho 5:19. Na katika huduma ndani ya hekalu lililo mbinguni, "Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminie asipotee, bali awe na uzima wa milele." Yohana 3:16.

Itaendelea tafadhari baki nasi.......

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.