Nimwambiaye Koreshi, Mchungaji wangu, naye atayatenda mapenzi yangu; hata ataunena Yerusalemu, Utajengwa; na hilo hekalu, Msingi wako utawekwa.
Isaya 44:28.
Bwana anazo rasilimali. Mkono wake upo kwenye vyombo vya serikali. Wakati ulipofika kwa ajili ya hekalu lake kujengwa upya, alimsukuma Koreshi kama wakala wake kuona unabii uliomhusu yeye mwenyewe na kuwapa Wayahudi uhuru wao.
Kuokolewa kwa Danieli kutoka kwenye tundu la simba kulitumiwa na Mungu kufanya mguso unaofaa akilini mwa Koreshi Mkuu….
Mfalme alipoona maneno yaliyotaja mambo kabla ya wakati, zaidi ya miaka mia moja kabla ya kuzaliwa kwake, namna Babeli itakavyochukuliwa; aliposoma ujumbe ambao aliandikiwa na Mtawala wa ulimwengu wote,…moyo wake uliguswa sana na akakusudia kutimiza utume wake wa kimbingu ambao alikuwa amepewa. Alikuwa awaweke huru mateka wa Yuda huru; alikuwa pia awasaidie kurejesha hekalu la Yehova. Kwenye tamko lilitangazwa “katika ufalme wake wote,” Koreshi alitangaza hamu yake ya kuwawezesha Waebrania kurudi na kujenga tena hekalu lao….
Habari njema za tamko hili zilifika hadi kwenye majimbo ya mwisho kabisa ya utawala wa mfalme na kila mahali kati ya watoto waliotawanyika kukawa na shangwe kuu. Wengi, kama Danieli, walikuwa wakijifunza unabii na walikuwa wakimwomba Mungu aingilie kati kwa niaba ya Sayuni….
Koreshi alimtwika jukumu Zerubabeli la kufanya kazi kama liwali wa kundi lililokuwa likirudi Yuda; pamoja naye pia alihusishwa kuhani mkuu Yoshua. Safari ndefu ya kupita kwenye jangwa pana ilikamilishwa kwa usalama na kundi lililokuwa na furaha… mara likaanza kazi ya kujenga upya kile kilichokuwa kimebomolewa na kuharibiwa.
Bwana Mungu mwenye uwezo wote anatawala. Wafalme wote, mataifa yote, ni vyake, chini ya utawala na serikali yake. Rasilimali zake hazina kikomo. Mwenye hekima anasema, “Moyo wa mfalme huwa katika mkono wa Bwana; Kama mifereji ya maji huugeuza po pote apendapo.” Wale ambao matendo yao yanashikilia hatima za mataifa, huwa wanatazamwa kwa uangalifu usiokoma na Yeye “awapaye wafalme wokovu.”
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon