KATIKA ROHO YA ELIYA



Naye atatangulia mbele zake katika roho ya Eliya, na nguvu zake, ili kuigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto, na kuwatilia waasi akili za wenye haki, na kumwekea Bwana tayari watu waliotengenezwa. Luka 1:17.

Mungu alikuwa amemuita mwana wa Zakaria kwa ajili ya kazi kubwa, kazi kuu ambayo mtu alipata kupewa… Yohana alikuwa aende mbele kama mjumbe wa Yehova ili kuwaletea watu nuru ya Mungu. Ilimpasa ayape mawazo yao mwelekeo mpya. Ilikuwa ni lazima awaguse kwa utakatifu wa matakwa ya Mungu na hitaji lao la haki yake kamilifu. Mjumbe wa namna hiyo ilipasa awe mtakatifu. Ilikuwa ni lazima awe hekalu ambamo Roho Mtakatifu anakaa. Ili aweze kukamilisha utume wake, ilikuwa ni lazima awe na afya nzuri kimwili, na nguvu za kiakili na za kiroho. Kwa sababu hiyo, ilikuwa muhimu kwake kwamba aweze kudhibiti tamaa ya chakula na hisia zake. Ilikuwa ni lazima aweze kudhibiti nguvu zote alizokuwa nazo ili apate kusimama kati ya watu akiwa hayumbishwi na mazingira kama miamba na milima ya jangwani iliyokuwa ikimzunguka.

Wakati wa Yohana Mbatizaji, uchu wa utajiri na kupenda starehe na hali za kujionesha vilikuwa vimeenea. Starehe za mapenzi, kula na kunywa, vilikuwa vikisababisha maradhi ya kimwili na upotovu, vinavyotia ganzi mitazamo ya kiroho na kupunguza uwezo wa kuhisi dhambi. Ilimpasa Yohana asimame kama mwanamatengenezo. Kwa maisha yake ya kujinyima na mavazi ya kawaida alikuwa akemee hali ya kutokuwa na kiasi ya wakati wake. Kwa namna hiyo, maelekezo yaliyotolewa kwa wazazi wa Yohana, -- somo la kiasi kutoka kwa malaika aliyetoka kwenye kiti cha enzi cha mbinguni….

Katika kuandaa njia kwa ajili ya ujio wa mara ya kwanza wa Kristo, alikuwa mwakilishi wa wale ambao inawapasa waandae watu kwa ajili ya kuja kwa Bwana mara ya pili. Dunia imetopea katika kuendekeza nafsi. Ubaya na kauli za uwongo zimezidi. Mitego inayoangamiza ya Shetani imeongezeka. Wale wote ambao wangekamilisha utakatifu katika kicho cha Mungu ni lazima wajifunze masomo ya kiasi na kujitawala nafsi. Hamu ya chakula na hisia ni lazima visalimishwe kwa uwezo wa juu wa akili. Hali hii ya kunidhamisha nafsi ni muhimu kwa nguvu ya kiakili na ufahamu wa kiroho ambavyo vitakuwezesha kutuelewesha na kutenda ukweli mtakatifu wa neno la Mungu. Kwa sababu hii kiasi kinapata nafasi yake katika kazi ya maandalizi ya kuja kwa Kristo mara ya pili.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text and food
Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
9 September 2019 at 04:07 delete

Asante, karibu pia tujifunze jinsi Roho ya Eliya inavyotenda kazi katika agano jipya..bofya link hii kusoma >> https://wingulamashahidi.org/2019/07/10/roho-ya-eliya-katika-agano-jipya-inatendaje-kazi/

Reply
avatar
Powered by Blogger.