USIKATE TAMAA MUNGU YUPO KWA AJILI YAKO.

Mtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza,
Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele. Zaburi 55:22.

Usipeleke matatizo yako kwa wanadamu. Yapeleke kwa Bwana. Unaweza kudhani kwamba inapasa wengine wakuhurumie ktk majaribu yako, lakini nyakati fulani utakatishwa tamaa. Kamwe Yesu hakatishi tamaa yeye ajaye kwake ili asaidiwe.

Anakwambia leo hii, "Njoni kwangu,... nami nitawapumzisha" (Mt 11:28). Atakupa pumziko ktk yeye. Hakuna ye yote ajaye kwake anayeondoka bila kusaidiwa. Peleka mizigo kwa Mbeba Mizigo wa Mbinguni na uiache kwake, ukijua kwamba atakubebea.

Fanyeni sehemu yenu ktk kujisaidia wenyewe, kama iwapasavyo kufanya wote wapendao kubarikiwa. Msidumu ktk shida za maisha ya Kikristo. Msiongee juu ya majaribu yenu..... msitamke hata neno moja la kukatisha tamaa, kwani maneno kama hayo umpendezesha shetani. Zungumzieni kuhusu uzuri wa Kristo na eleza juu ya uwezo wake. Ni rahisi kusema maneno ya tumaini na imani na ujasiri kama ilivyo maneno ya malalamiko.

Adui anapokwambia kwamba Bwana amekuacha, mwambie kwamba unajua kwamba hajakuacha; kwani anasema, "Sitakupungukia kitu kabisoa, wala sitakuacha kabisa" (Ebr 13:5). Mfukuze Adui. Mwambie kwamba hutamwaibisha Bwana kwa kutilia mashaka upendo wake....

Msaada ambao Mwokozi yuko tayari kutupatia hauna mpaka. Anatuomba tuingize maishani mwetu neema ambayo itatutunza tusitende dhambi. Kutoka msabani kalvari; uhuru, tumaini na nguvu vinatujia. Usimfedheheshe Mkombozi wako kwa kutilia mashaka uwezo wake. Mwamini wakati wote. Shikilia utajiri wa neema yake, ukisema, "Nitaamini; ninaamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yangu." Mbele yako, njia inaweza kuonekana kuwa giza, lakini Yesu anaweza kuifanya iwe nuru.

Huku mkimtwika Yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu. 1 Petro 5:7


Image may contain: 1 person, text and closeup

Previous
Next Post »
Powered by Blogger.