ELIYA MBELE YA AHABU



Naye akajibu, Si mimi niliyewataabisha Israeli; bali ni wewe, na nyumba ya baba yako, kwa kuwa mmeziacha amri za Bwana; nawe umewafuata mabaali.
1 Wafalme 18:18.

Kwa miaka migumu ya ukame na njaa, Eliya aliomba kwa dhati kwamba mioyo ya Israeli igeuke kutoka kwenye ibada ya sanamu na kuelekea kwenye utiifu kwa Mungu. Nabii alisubiri kwa uvumilivu, wakati mkono wa Bwana ukiwa mzito sana juu ya nchi iliyopigwa….

Hatimaye, “baada ya siku nyingi,”neno la Bwana likamjia Eliya, “Enenda, ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi.”…

Mfalme na nabii wakasimama ana kwa ana. Japo Ahabu alikuwa amejawa na chuki kali, bado mbele za Eliya alionekana kukosa nguvu. Kulingana na maneno yake ya kwanza yenye kuonesha kusita, “Je! Ni wewe, ewe mtaabishaji wa Israeli?” alidhihirisha bila kufikiria sawa sawa hisia za ndani kabisa za moyo wake. Ahabu akajua kwamba ilikuwa ni kutokana na neno la Mungu kwamba mbingu zilikuwa kama shaba, hata hivyo alitafuta kumtupia nabii lawama kutokana na hukumu nzito zilizoikalia nchi…

Huku akisimama katika hali ya kutokuwa na hatia mbele za Ahabu, Eliya hakujaribu kutafuta kisingizio au kumvika mfalme kilemba cha ukoka. Wala hakujaribu kuepuka hasira ya mfalme kwa habari njema kwamba ukame umekaribia kuisha. Hakuomba radhi kwa lolote. Akiwa na uchungu na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu, alimrudishia shutuma Ahabu, akimtamkia mfalme bila hofu kuwa ilikuwa ni dhambi zake na dhambi za baba zake, ambazo ziliiletea Israeli janga hili la kutisha…

Lipo hitaji leo la sauti yenye kemeo kali; kwani dhambi za kutisha zilikuwa zimewatenganisha watu na Mungu… Mahubiri laini yanayotolewa mara kwa mara hayaweki mguso wa kudumu; tarumbeta haitoi mlio unaoeleweka. Watu hawaguswi mioyoni kwa kweli zilizo wazi zinazopenya za neno la Mungu…

Mungu anaita watu kama Eliya, Nathani na Yohana Mbatizaji – watu watakaoubeba ujumbe wake kwa uaminifu, bila kujali matokeo; watu watakaonena ile kweli kwa ujasiri, hata pale inapopasa kujitoa kwa vyote alivyo navyo mtu.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: 1 person
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.