Mwokozi alipenda kuwadhihirishia wanafunzi wake kwamba, watu wa mataifa ni watu sawa na wengine wastahilio kuhesabiwa sawa sawa na watu wote, kama Wayahudi ambao hustahili kuwa na ahadi zile zile zipatikanazo kwa injili. (Waefeso 3:6).
Hivyo Kristo aliwafundisha wanafunzi wake kuwa ktk ufalme wa Mbinguni, hakuna mipaka ya nchi, wala hakuna ubaguzi wa rangi au kabila. Watu wote wa ulimwengu lazima wasikie injili ya neema ya upendo wa Mungu. Lakini hawakuelewa mambo hayo mpaka baadae ndipo walifahamu kuwa Mungu alifanya watu wote kuwa wa damu moja: watu wa kila taifa wakae ktk nchi. (Matendo 17:26).
Wanafunzi hawa wa kwanza walikuwa na tabia za namna mbali mbali. Ingawa walikuwa na tabia tofauti, lakini walipaswa kuwa ktk umoja bila kutofautiana. Kwa namna alivyokuwa Kristo alitaka kuwaunganisha ktk umoja naye. Mzigo wake kuwahusu ulionekana ktk sala yake aliyowaombea kwa Baba; akisema: "Wawe na umoja ili ulimwengu upate kujua kuwa wewe ndiwe uliyenituma; na umewapenda wao kama ulivyonipenda mimi"
(Yohana 17:21-23). Alijua kuwa ukweli utashinda ktk ulimwengu, na bendera yake yenye damu siku moja itapepea kwa wanafunzi wake.
Kristo alipokumbuka wakati ujao atawaacha peke yao wakiendesha kazi, alitaka kuwatayarisha kukabiliana na wakati ujao.
Alijua kuwa watapambana na mateso makali watafukuzwa ktk masinagogi na kutiwa gerezani. Baadhi yao watauawa.
Akizungumza mambo yahusuyo wakati ujao, alitaka wakati huo wayakumbuke maneno yake na kujiimarisha wenyewe ktk Mwokozi.
Alisema "Msifadhaike mioyoni mwenu naenda kuwaandalia mahali. Na nikienda kuwaandalia mahali nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi nanyi muwepo" (Yohana 14:1-3). Nikienda zangu nitaendelea kufanya kazi pamoja nanyi. Naenda kwa Baba yangu na Baba yenu pia ili kuunganika naye kwa ajili yenu.
Aniaminie mimi kazi nizifanyazo na yeye atafanya, na kubwa zaidi, kwa kuwa naenda kwa Baba (Yohana 14:12). Kristo hakuwa na maana kuwa wanafunzi wanafanya makuu zaidi ya kujivuna, la, ila kazi yao itakuwa na ukubwa zaidi. Alisema kuwa hali hiyo itawahusu wote watakaofanya kazi wakiongozwa na Roho Mtakatifu.
MUWE NA PUMZIKO JEMA LA SABATO.

EmoticonEmoticon