“Kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lo lote, wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahauliwa.”
Mhubiri 9:5.
Sauli alipoomba azungumze na Samweli, Bwana hakumfanya Samweli amtokee. Hakuona chochote. Shetani hakuruhusiwa kuvuruga pumziko la Samweli kaburini, na kwa hakika kumpandisha kwa mchawi wa Endori. Mungu hampi shetani mamlaka ya kufufua wafu. Lakini malaika wa Shetani huchukua mwonekano wa marafiki zetu waliokufa, wakizungumza na kufanya vitendo kama wao, ili kupitia kwa hao wanaojifanya kuwa marafiki zetu waliokufa atekeleze kazi yake ya Udanganyifu. Shetani alimjua Samweli fika, na alijua namna ya kumwigiza mbele ya mchawi wa Endori, na kutamka kwa usahihi yale yatakayompata Sauli na wanawe.
Shetani atakuja kwa namna inayokubalika sana ili apate kudanganya, na atajifanya kujali mambo yao, na kuwapotosha toka kwa Mungu bila hata wao kujua. Anawaweka chini ya udhibiti wake, mwanzoni kwa tahadhari, mpaka pale uwezo wao wa kugundua unapoishiwa nguvu kabisa. Ndipo sasa hutoa mapendekezo kwa ujasiri, hadi pale anapoweza kuwafanya kutenda karibia kiwango chochote kile cha makosa. Anapowafikisha kikamilifu katika mitego yake, ndipo anapenda waone mahali walipo, na kufurahia kuona kule kuchanganyikiwa kwao kama ilivyokuwa kwa suala la Sauli. Sauli alikuwa amemruhusu Shetani kumfanya mateka wake wa hiari, na sasa Shetani anaweka bayana maelezo sahihi ya mustakabali wa Sauli. Kwa kumpa Sauli maelezo sahihi ya mwisho wake, kupitia kwa mwanamke wa Endori, Shetani anafungua njia ya Israel kuongozwa na hila zake, ili kwa kumwasi Mungu, wamjue Shetani, na hivyo akate kitu cha mwisho ambacho kinawaunganisha na Mungu.
Sauli alijua kwamba katika kitendo hiki cha mwisho cha kumwendea mganga(mwaguzi), alikata kamba ya mwisho iliyomuunganisha na Mungu. Alijua kwamba kama awali hakujitenga na Mungu kwa kukusudia, kitendo hiki kilihitimisha utengano huo. Alikuwa amefanya mapatano na kifo, agano na kuzimu. Kikombe cha maovu yake kilikuwa kimejaa.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon