“Akawaambia, Si kazi yenu kujua nyakati wala majira, Baba aliyoyaweka katika mamlaka yake mwenyewe.”
Matendo 1:7.
Mchawi wa Endori alikuwa na makubaliano na Shetani kufuata njia yake katika mambo yote; ili shetani amfanyie miujiza na maajabu, na kumfunulia mambo ya faragha sana, ikiwa tu atajisalimisha kikamilifu kutawaliwa na mamlaka ya kishetani. Na hilo alilitenda.
Kwa utabiri wa kuangamia kwa Sauli, uliotolewa kupitia kwa mwanamke wa Endo, Shetani alikusudia kuwatega watu wa Israeli. Alitumaini kwamba wangemwamini mwaguzi huyu na hivyo kutafuta ushauri kwake. Hadaa anayotumia Shetani kuwavuta makutano ni kujifanya ana uwezo kuondoa pazia linaloficha mambo ya usoni na kuwafunulia wanadamu kile ambacho Mungu ameficha. Mungu ametufunulia katika neno lake matukio makuu yajayo katika siku za usoni—yote ambayo ni muhimu kwetu kuyajua—na ametupatia njia ya kusimama salama katikati ya hatari zote; lakini ni kusudi la Shetani kuua imani ya watu kwa Mungu, kuwafanya kutoridhika na hali zao za maisha, na kuwafanya kutaka kujua kile ambacho kwa hekima Mungu amewaficha, na kudharau kile alichofunua katika Neno lake.
Kuna wengi ambao wanakosa utulivu wa moyoni kabisa pale wanaposhindwa kuelewa matokeo halisi ya mambo yao. Hawawezi kustahimili kutokuwa na uhakika, na katika kukosa saburi kwao wanakataa kungoja ili waone wokovu wa Mungu. Shida zinazowapata zinawapeleka mpaka karibia kuiacha njia. Wanatoa fursa kwa hisia zao za kuasi, na kukimbia huku na kule katika huzuni kubwa, wakitafuta ufahamu juu ya kile ambacho hakijafunuliwa. Kama wangemwamini Mungu, na kukesha wakiomba, wangepata faraja ya kimbingu. Roho zao zingetulizwa na mawasiliano yao na Mungu. Waliochoka na kulemewa na mizigo wangepata raha nafsini mwao kama tu wangemwendea Yesu; Bali wanapopuuzia njia ambazo Mungu ameweka kwa ajili ya faraja yao, na kutafuta vyanzo vingine, wakitafuta kujua kile ambacho Mungu amezuilia, wanatenda dhambi ya Sauli, na hapo wanaambulia ujuzi wa mabaya tu.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon