KUJIUA



“Haki yake mtu mkamilifu itamwongoza njia yake; Bali mtu mwovu ataanguka kwa uovu wake.”
Mithali 11:5.

Katika uwanda wa Shunemu na mitelemko ya Mlima Gilboa majeshi ya Israeli na yale ya adui Wafilisti walikaribia ili kuanza vita kali. Ingawa matukio ya kutisha katika pango la Endori yalikuwa yameondoa matumaini yote toka moyoni, Sauli alipigana kufa na kupona kulinda kiti chake cha utawala na ufalme wake. Lakini jitihada yote hiyo ilikuwa bure. “Nao watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Wafilisti, wakaanguka wameuawa katika mlima wa Gilboa.” Wana watatu wa mfalme waliokuwa jasiri wakauawa. Wapiga upinde wakamkaribia Sauli. Alikuwa ameona askari wake wakianguka chini pande zake zote na wanawe watatu wakiuawa kwa upanga mbele zake. Akiwa amejeruhiwa hakuweza kupigana wala kukimbia. Kukimbia hakukuwezekana, naye akikusudia kutochukuliwa mateka na Wafilisti, akamwagiza mbeba silaha wake, “Futa upanga wako, unichome nao”. Mtu yule alipokataa kumwinulia mkono mtiwa mafuta wa Bwana, Sauli alijiua mwenyewe kwa kuangukia upanga wake. Hivyo mfalme wa kwanza wa Israeli akaangamia, akiwa na hatia ya kujiua nafsini mwake.

Kwa kufuata matakwa ya Shetani, Sauli alikuwa akiharakisha mwenyewe matokeo yale yale ambayo kwa uwezo usiotakaswa alikuwa akijitahidi kuyabadilisha.

Mashauri ya Bwana yalikuwa yamepuuziwa tena na tena na mfalme mwasi, na Bwana alikuwa amemwacha aangamie katika upumbavu wa hekima yake mwenyewe. Mvuto wa Roho Mtakatifu ungemzuia kuiendea njia ya uovu ambayo alikuwa ameichagua, ambayo hatimaye ilileta uangamivu wake. Mungu anachukia dhambi zote, na pale mtu anapodumu kukataa mashauri yote ya mbingu, anaachwa katika udanganyifu wa adui, ili avutwe mbali na tamaa yake na kudanganyika.

Mfalme wa kwanza wa Israeli alishindwa, kwa kuwa aliweka matakwa yake juu ya matakwa ya Mungu. Kupitia kwa nabii Samweli Bwana alimwelekeza Sauli kwamba kama mfalme wa Israel utendaji wake wote lazima uwe na uadilifu usioyumba. Ndipo Mungu angeibariki serikali yake kwa kuipatia mafanikio. Lakini Sauli alikataa kufuata utii kwa Mungu kuwa kipaumbele chake, na kanuni za mbinguni kiongozi wa mwenendo wake. Alikufa kwa aibu na kukata tamaa.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.