RAFIKI AOMBOLEZA



“Jinsi mashujaa walivyoanguka, na silaha za vita zilivyo-angamia!”
2 Samweli 1:27.

Mara mbili Daudi alikuwa amepata nafasi ya kumwua Sauli; lakini walipomtaka amwue, alikataa kumwinulia mkono yeye aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Amri ya Mungu kuitawala Israeli . . .

Huzuni ya Daudi kwa kifo cha Sauli ilikuwa ya dhati na kubwa, ikidhihirisha wema adilifu. Hakufurahia kuanguka kwa adui yake. Kikwazo ambacho kilizuia njia yake ya kuendea kiti cha ufalme wa Israeli kiliondolewa, lakini hili halikuwa la kumfurahisha. Kifo kilikuwa kimefuta kabisa kumbukumbu ya ukatili na kutoaminiwa na Sauli, na sasa hakukumbuka chochote juu ya hicho katika historia isipokuwa yale yaliyokuwa mema na ya kifalme, jina la Sauli lilihusianishwa na lile la Yonathani, ambaye urafiki baina yao ulikuwa wa dhati na usio na ubinafsi.

Yonathani, mrithi wa kiti cha ufalme kwa haki ya kuzaliwa, lakini kwa kujua kwamba Mungu amemtenga Daudi kwa ajili hiyo, aliyekuwa rafiki yake mpendwa, akikinga maisha ya Daudi katika kuhatarisha maisha yake mwenyewe; thabiti upande wa baba yake katika nyakati mbaya za kudhoofu kwa utawala wake, na akiwa kando yake, akifa hatimaye – Jina la Yonathani ni la thamani sana mbinguni, na ni ushahidi duniani wa kuwepo kwa pendo lisilo na ubinafsi na nguvu ya pendo la aina hiyo.

Wimbo ambao Daudi anaelezea hisia za moyo wake ukawa wa thamani sana kwa taifa lake, na kwa watu wa Mungu katika zama zote zilizofuata….

“Jinsi mashujaa walivyoanguka Katikati ya vita!

Ee Yonathani, wewe umeuawa

Juu ya mahali pako palipoinuka

Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu,

Ulikuwa ukinipendeza sana;

Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,

Kupita upendo wa wanawake.

Jinsi mashujaa walivyoanguka,

Na silaha za vita zilivyoangamia! “

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.