NI LAZIMA WANAWAKE WATHIBITISHE KIWANGO CHA JUU CHA TABIA/MWENENDO:
Naandika kwa moyo wenye HUZUNI ya kwamba WANAWAKE katika zama hizi, walioolewa pamoja na wasioolewa, mara nyingi sana hawadumishi akiba ambayo ni ya muhimu.
Wanatenda kama WANAOJIUZA. Wanawahamasisha umakini wa Wanaume wasiooa na wale waliooa, na wale walio dhaifu katika nguvu ya kimaadili WATANASWA.
Vitu hivi, ikiwa vitaruhusiwa, HUUA hisia MAADILI na KUPOFUSHA Akili ili UOVU Usionekane kuwa na dhambi.
Fikra huamshwa ambavyo zisingalikuwa kama mwanamke ANGETUNZA mahali pake katika STAHA na UTULIVU.
Asingeweza kuwa na LENGO au MSUKUMO ulio kinyume cha sheria yeye mwenyewe, bali ingekuwa ametia moyo kwa Wanaume waliojaribiwa, na wanaohitaji msaada wote wanaoweza kuupata kutoka kwa wale wanaohusiana nao.
Kwa kuwa Mwangalifu, Mtulivu, asiye na mazoea yaliyopitiliza, asiyepokea mivuto isiyo na sababu [za msingi], bali wakitunza sauti yenye maadili ya juu na kuwa wenye HESHIMA, Uovu ungeweza KUEPUKIKA.
Kwa muda mrefu nimekuwa nikipanga kuongea na dada zangu na kuwaambia kwamba, kutokana na kile Mungu amekuwa AKIPENDEZWA kunionyesha wakati baada ya wakati, kuna kosa kubwa miongoni mwao.
Hawapo Makini kuacha kutokana na MWONEKANO wote wa dhambi.
Sio wote walio waangalifu katika mwenendo wao, kadri wanavyokuwa Wanawake Wanaokiri uchaji Mungu.
Maneno yao SIO mazuri na yaliyochaguliwa vizuri kama yale ya wanawake ambao wamepokea neema ya Mungu IWAPASAVYO kuwa.
Wamezoeana sana na wapendwa wao. Wakiwazunguka kwa karibu, wakiinama kuelekea kwao, na huonekana kuchagua jamii yao.
Wametoshelezwa sana na mvuto wao. Kutokana na Nuru ambayo Mungu amenipatia, dada zetu wanapaswa kuchukua NJIA TOFAUTI Sana.
Wanapaswa kuwa Waliojitunza zaidi, wasiionyesha jeuri, na kujipa moyo ndani yao wenyewe "Wenye kuona haya na UTULIVU."
Ndugu pamoja na akina dada hujitia katika maongezi yenye uchangamfu kupita kiasi wanapokuwa katika jamii ya kila mmoja.
Wanawake wanaokiri uchaji Mungu wanajitia katika DHIHAKA, MZAHA na UCHESHI zaidi.
Hii HAIFAI na humhuzunisha Roho wa Mungu. Maonyesho haya hudhihirisha UKOSEFU wa usafi wa kweli wa Kikristo.
Hawaimarishi roho katika Mungu, bali huleta giza; wanawafukuzia mbali malaika halisi, waliosafishwa wa mbinguni na kuwaweka chini wale ambao hushughulika katika makosa haya mpaka kwenye kiwango cha chini.
Wanawake MARA NYINGI SANA ni WANAOTIA [watu] MAJARIBUNI. Katika Ulaghai mmoja ama mwingine WANAVUTIA umakini wa Wanaume waliooa na wasiooa, na kuwaongoza mpaka WANAVUNJA sheria ya Mungu, mpaka Ufanisi wao unapoharibiwa, na roho zao zinapokuwa katika HATARI….
Kama wanawake wangeyainua maisha yao tu, na kuwa watendakazi pamoja na KRISTO, kungekuwa na hatari ndogo sana kupitia ushawishi wao;
lakini kwa hisia walizonazo za KUTOJALI kulingana na uwajibikaji wa nyumbani na kulingana na madai kwamba Mungu yupo juu yao,
Ushawishi wao mara nyingi UNA NGUVU katika UELEKEO USIO SAHIHI, uwezo wao hudumazwa, na kazi zao hazibebi mvuto wa kimbingu.
Adventist Home uk 55 (1952)

EmoticonEmoticon