Wapendwa tusisikilize maneno ya watu ambao wanadanganya watu kuwa hakuna haja ya kushika Sheria ili kuingia Mbinguni. Hao ni waalimu wa Uongo na ambao wanatumiwa na Ibilisi kudanganya watu. Shetani ana hasira na chuki kali dhidi ya hao wanaotunza Amri za Mungu na Imani ya Yesu. Kitabu cha Ufunuo kinamwonyesha Shetani kama Jemedari Mkuu wa vita anayewaongoza wana wa Uasi ili kufanya vita dhidi ya wale wazitunzao Amri za Mungu na kuwa na Ushuhuda wa Yesu. Biblia yasema hivi: “Joka akamkasirikia yule mwanamke, akaenda zake afanye vita juu ya wazao wake waliosalia, wazishikao amri za Mungu, na kuwa na ushuhuda wa Yesu; naye akasimama juu ya mchanga wa bahari. [Ufu12:17].
Vita kuu ni kati ya wema na Uovu na kati ya Kristo na shetani. Lakini Tunatambua Mema kutokana na kanuni kuu ya Wema yaani Amri kumi za Mungu. Ni Amri kumi zinazofunua wema, haki, Utakatifu, na Upendo wa Mungu. Mtume Paulo aliandika hivi kuhusu Amri kumi: “Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. [War7:12] . Na tena Mtume Paulo akaandika hivi kuhusu Amri kumi: “Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako [Warumi 13:8-9]. Hivyo huwezi kuwa mwema, Mwenye haki, na Mtu mtakatifu, na Mtu mwenye Upendo bila kuzishika zile Amri kumi.
Kile anachofanya Shetani ni kuwaongoza watu kuziasi na kuzichukia Amri kumi, anajua kuwa hawawezi kuwa wema, wenye upendo, watakatifu, na wenye haki kwani Maana ya dhambi hasa ni kuvunja Sheria za Mungu. Kazi ya Yesu ni kutoa msamaha wa dhambi kwa wavunjaji wa sheria za Mungu, na kuwapa Neema na uwezo wa kuzitii tena Sheria za Mungu. Kazi ya shetani ni kinyume na ile ya Yesu. Shetani anawaongoza watu kuziasi sheria za Mungu na hivyo kuikataa Neema yake. Wengine anawaongoza kuzivunja Amri zote kumi, na wengine anawaongoza kupuuza amri moja tu kati ya zile kumi. Anajua kuwa kila avunjaye Amri kumi hata moja tu, hawezi kamwe kuokolewa na Yesu ama kuurithi uzima wa milele. Biblia yasema hivi: “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Kwa maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekuwa mvunja sheria. [Yak2:10-11]
Uchaguzi ni wako.

EmoticonEmoticon