HAKUNA JIBU TOKA KWA MUNGU



“Lakini Sauli alipouliza kwa BWANA, BWANA hakumjibu, wala kwa ndoto, wala kwa Urimu, wala kwa manabii.”
1 Samweli 28:6.

Kamwe Mungu haitupi roho inayomjia kwa dhati na unyenyekevu wa moyo. Kwa nini hakumjibu Sauli? Kwa kitendo chake mfalme alikuwa amepoteza manufaa ya njia zote kuwasiliana na Mungu. Alikuwa ameyakataa mashauri ya nabii Samweli; alikuwa amemfanya Daudi, mteule wa Mungu, mkimbizi; alikuwa amewachinja makuhani wa Bwana… alikuwa ametupilia mbali Roho wa neema, je angeweza kujibiwa kwa ndoto na maono? Sauli hakumgeukia Mungu kwa roho ya toba na unyenyekevu. Alichotaka hakikuwa msamaha kwa ajili ya dhambi na kupatanishwa na Mungu, bali kuokolewa dhidi ya adui zake. Kwa ukaidi wake na roho yake ya uasi alikuwa amejitenga na Mungu. Kusingekuwa na njia nyingineyo ya kurejea isipokuwa toba ya dhati na majuto; lakini mfalme mwenye kiburi, katika kilio chake na kukata tamaa aliazimia kutafuta msaada kwingineko…. mfalme alijulishwa kuwa mwanamke aliyekuwa na roho ya uaguzi aliiishi Endo mafichoni… Akijibadilisha kwa mavazi, Sauli alimwendea usiku akiambatana na wasaidizi wake wawili kutafuta msaada kwa mganga . . .

Utumwa wa kutisha kiasi gani kama wa yule aliyejitoa atawaliwe na kilicho kibaya katika ukatili wote—nafsi yake mwenyewe! Kumtumainia Mungu na kutii mapenzi yake ndiyo masharti pekee ya kumfanya Sauli kuwa mfalme wa Israel. Kama angefanya hivyo muda wote wa utawala wake; utawala wake ungekuwa salama; Mungu angekuwa kiongozi wake, Aliye mweza wa yote angekuwa ngao yake. Mungu alikuwa amemvumilia sana Sauli; na ingawa uasi wake na ukaidi vilikuwa vimekaribia kabisa kuzima sauti ya Mungu katika roho yake, bado alikuwa na nafasi ya toba. Lakini katika shida yake alipomwacha Bwana na kwenda kutafuta msaada kwa wakala wa Shetani, alikata kamba ya mwisho iliyokuwa ikimuunganisha na Muumba wake . . .

Kwa kutafuta msaada kwa roho ya giza Sauli alijiangamiza mwenyewe. Akiteseka kwa hofu ya kukata tamaa, isingewezekana kwake kuongoza jeshi kwa ujasiri. Akiwa ametengwa na chanzo cha nguvu, asingeweza kuelekeza mioyo ya kumtazama Mungu kama msaada wao. Hivyo utabiri wa maovu ukapata fursa ya kutimia.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.