KISASI CHA MUNGU



“Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.”
Warumi 12:19.

Ingawa Nabali alikataa kumsaidia Daudi na watu wake katika uhitaji wao, lakini usiku ule alifanya sherehe ya kifahari kwa ajili yake na marafiki zake wavunja sheria, na akajiingiza katika kula na kunywa mpaka akazama katika usingizi wa ulevi.

Nabali hakuona ubaya wowote kuponda mali yake katika anasa na kujitukuza; lakini ilionekana kujinyima kunakoumiza sana kwake kuwafidia wale ambao wamekuwa kama ukuta kwa wachungaji na mifugo yake. Nabali alikuwa kama yule tajiri katika mfano wa tajiri. Alifikiria jambo moja tu, kutumia mali aliyopewa na Mungu katika kukuza matakwa na hamu zake za kibinafsi. Hakufikiria kumshukuru mtoaji. Hakuwa tajiri kwa mambo ya Mungu; maana hakuvutwa na hazina ya milele. Anasa za sasa, mapato ya wakati huu ndiyo mawazo yaliyomtawala. Hicho ndicho kilikuwa mungu wake.

Nabali alikuwa mtu mwoga; na alipogundua jinsi ambavyo upumbavu wake ulikuwa umempeleka karibu na kifo cha ghafla, alionekana kupatwa na ugonjwa wa kupooza. Akiogopa kwamba bado Daudi atamlipiza kisasi, alijawa na hofu na kuzama katika hali ya kupooza kusiko na matumaini. Baada ya siku kumi akafa. Maisha ambayo Mungu alikuwa amempa yaliishia kuwa laana kwa ulimwengu. Katikati ya kustarehe kwake, Mungu alikuwa amemwambia, kama alivyomwambia yule tajiri katika mfano alioutoa Yesu, “Usiku huu wanataka roho yako…” (Luka 12:20).

Daudi alipopata habari za kifo cha Nabali, alishukuru kuwa Mungu alikuwa amelipiza kisasi mwenyewe. Alikuwa amezuiliwa asitende mabaya, na Bwana alikuwa amerejesha maovu ya mwovu katika kichwa chake mwenyewe. Katika utendaji huu wa Mungu kwa Nabali na Daudi, watu wanatiwa moyo kumkabidhi Mungu mambo yao, maana kwa muda wake mwafaka atayanyoosha mambo yote…

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.