Nakuomba ulisamehe kosa lake mjakazi wako, kwa kuwa hakika BWANA atamfanyia bwana wangu nyumba iliyo imara, kwa sababu bwana wangu anavipiga vita vya BWANA; tena uovu hautaonekana ndani yako siku zako zote.
1 Samweli 25:28.
Abigaili alikutana na Daudi kwa heshima, akimwonesha heshima na uungwana, na kupeleka ombi lake kwa maneno mazuri yaliyopata kibali. Bila kupuuzia ufidhuli wa mume wake, bado akasihi apate nafasi ya kuendelea kuishi. Alidhihirisha pia ukweli kwamba hakuwa mtu mwenye busara tu, bali mwanamke mcha Mungu, anayezifahamu kazi na njia za Mungu katika maisha ya Daudi. Alikiri imani yake thabiti kwamba Daudi alikuwa mtiwa mafuta wa Bwana.
Matendo ya Abigaili yalimwashiria Daudi njia aliyopaswa kufuata. Anapaswa kupigana vita vya Bwana. Hakupaswa kutafuta kulipiza kisasi kwa makosa ya mtu binafsi, hata kama angeudhiwa kama msaliti… Maneno haya yangetoka tu midomoni mwa yule aliyepata hekima kutoka juu. Ucha Mungu wa Abigaili, kama harufu nzuri ya maua, ulisambaa bila yeye kujua kwa njia ya mwonekano wa uso wake, maneno na matendo yake. Roho wa Mwana wa Mungu alikuwa anakaa ndani ya roho yake. Maneno yake, yakikolezwa na neema, yaliyojaa wema na amani, yalileta mvuto wa mbinguni. Mawazo bora zaidi yakamjia Daudi, na akaogopa sana alipofikiria juu ya matokeo ambayo yangesababishwa na utendaji wake wa kukurupuka . . . .
Maisha ya Kikristo ambayo yamewekwa wakfu kwa Mungu daima huleta nuru, faraja na amani. Yana sifa ya usafi, umahiri, usahili, na manufaa. Yanatawaliwa na ule upendo usio na ubinafsi unaoleta mvuto mtakatifu. Yamejaa Kristo, yanaacha njia ya nuru popote Mkristo huyo anapopita.
Abigaili alikuwa mshauri na mwonyaji mwenye hekima. Hasira ya Daudi ilitokomea chini ya mvuto na hoja za Abigaili . . .
Kwa moyo wa unyenyekevu alipokea maonyo… alitoa shukurani na mibaraka kwa vile alimshauri kwa haki. Wako wengi ambao, wanapoonywa, wanaona itampa sifa mtoaji kama watakubali maonyo bila kushindwa kujizuia; lakini ni wachache kiasi gani hupokeo maonyo kwa shukurani ya moyo na kuwabariki wale wanaojitahidi kuwazuia kuiendea njia ya mabaya.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon