Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mithali 31:30.
Katika tabia ya Abigaili, mke wa Nabali, tunapata kielelezo cha mwanamke amchaye Kristo; wakati ambapo mume wake anadhihirisha anavyokuwa mtu aliyejisalimisha chini ya utawala wa Shetani.
Daudi alipokuwa mkimbizi mbele za Sauli, aliweka kambi karibu na mali ya Nabali, na alikuwa amewalinda wachungaji na mifugo ya mtu huyu… Katika wakati wa uhitaji, Daudi akatuma watumishi kwa Nabali na ujumbe wa kiungwana, akiomba chakula kwa ajili yake na watu wake, na Nabali akamjibu kwa jeuri, akilipa uovu kwa wema, na kukataa kushiriki utajiri wake na jirani zake. Hakuna ujumbe wa heshima kama ule ambao Daudi alimtumia Nabali, lakini mtu huyu akamsingizia Daudi ili kuhalalisha uchoyo wake, akiwasema Daudi na watu wake kama watumwa waliotoroka. Mjumbe aliyetumwa aliporejesha kauli hii ya kifudhuli, hasira ya Daudi ikawaka, akadhamiria kulipiza kisasi mara moja. Mmoja wa watumishi wa Nabali, akihofia ufidhuli wa Nabali kuleta matokeo mabaya, akaja na kumjulisha mke wa Nabali, akijua kuwa alikuwa na roho tofauti na ya mume wake, na alikuwa mwanamke mwenye busara sana…
Abigaili akaona kwamba sharti kitu fulani kifanyike kuepushia mbali matokeo ya makosa ya Nabali, na kwamba hana budi kufanya kitu kwa haraka bila hata kushauriana na mume wake. Alijua kwamba kushauriana naye hakutasaidia, maana mapendekezo yake yangepokelewa kwa matusi na dharau. Angemkumbusha kwamba yeye ndiye mkuu wa kaya, na kwamba yeye alikuwa mkewe, na hivyo anapaswa kumtii, na kutenda kama mumewe asemavyo…
Bila idhini ya mume wake, akakusanya vitu kwa kadri alivyoamini vitahitajika kwa ajili ya kujipatanisha na hasira ya Daudi; maana alijua kuwa Daudi alidhamiria kulipiza kisasi kwa kutukanwa kwake… Jinsi hii ya utendaji wa Abigaili katika jambo hili ilipata kibali cha Bwana, na mazingira haya yalifunua roho na tabia ya uungwana aliyo nayo.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon