YESU KWETU NI RAFIKI

HISTORIA YA WIMBO NO: 282 Ktk Vitabu Vikubwa,


Wimbo huu ulitungwa na Joseph M Scven Ambaye alizaliwa mwaka 1819 na kufa mwaka 1886

Wimbo huu aliuandika mwaka 1855 ambapo alikuwa ana mfariji mama yake alipokuwa IRELAND wakati yeye akiwa Canada
Maneno ya wimbo huu aliyapata ktk biblia Yohana15:13 inasema hakuna mwenye upendo kama huu mtu kuutoa uhai wake kwaajili ya rafiki. na kutoka33:11 nk. mtunzi hakuona rafiki mwingine zaidi ya Yesu.

Mwaka 1868 wimbo huu ulipangiliwa kimusic na Charles Crozat Converse ambaye alizaliwa mwaka 1832 na kufa mwaka 1918,
Wimbo huu ulisikika Japan mwaka 1910 na kuandikwa Kijapan
pia ulifika indonesia
na wimbo huu uliimbwa mwanzoni mwa vita ya kwanza ya dunia ili kuwasogeza watu kwa Yesu watu wengi walimpokea Yesu kupitia wimbo huu na ulienea kwa kasi sana mpaka kutufikia sisi,

ni wimbo wa matumaini ktk kingereza ni what a friend we have in Jesus 

Image may contain: one or more people
Previous
Next Post »

1 comments:

Write comments
kisaliah
AUTHOR
20 April 2019 at 23:27 delete

pia nilitaka nipate historia ya wimbo wa tarumbeta ya mwana

Reply
avatar
Powered by Blogger.