USHINDI NI KATIKA JINA LA YESU.



Ushindi na utii wa Kristo ni ule wa kibinadamu halisi. Ktk maamuzi yetu, tunafanya makosa mengi kwa sababu ya misimamo yetu yenye makosa kuhusu ubinadamu wa Bwana wetu. Tunapoupa ubinadamu wake nguvu ambayo haiwezekani kwa mwanadamu kuwa nayo ktk mapambano yake na Shetani, basi, tunaharibu utimilifu wa ubinadamu wake. Neema yake pamoja na nguvu zake anawapa wale wote wanaompokea kwa imani.

Bwana anadai sasa kwamba kila mwana na binti ya Adamu, kwa njia ya imani ktk Yesu Kristo, apate kumtumikia ktk ubinadamu wake ambao tunao hivi sasa. Bwana Yesu ameliziba lile shimo kubwa ambalo lilisababishwa na dhambi. Ameiunganisha mbingu na dunia, wanadamu wasiodumu na Mungu wa milele. Yesu, Mkombozi wa ulimwengu, aliweza kuzishika amri (Kumi) za Mungu kwa njia ile ile ambayo wanadamu wote wanaweza kuzishika. 7BC 929.

Hatupaswi kumtumikia Mungu kana kwamba sisi hatukuwa binadamu, bali tunapaswa kumtumikia Yeye ktk hali ya kibinadamu tuliyo nayo, ambayo imekombolewa na Mwana wa Mungu; kwa njia ya haki ya Kristo tutasimama mbele za Mungu tukiwa tumesamehewa, na kuwa kana kwamba hatukufanya dhambi kamwe. 5BC 1142.

Ubinadamu wa Mwana wa Mungu ni kila kitu kwetu. Ni mnyororo ule wa dhahabu unaozifunga roho zetu kwa Kristo, na kwa njia yake Kristo {zinafungwa} kwa Mungu.-- 1SM 244.


No automatic alt text available.

Previous
Next Post »
Powered by Blogger.