“WALA HAKUWAZUIA”



“Kwa maana nimemwambia ya kwamba nitaihukumu nyumba yake milele, kwa ajili ya ule uovu alioujua; kwa kuwa wanawe walijiletea laana, wala yeye hakuwazuia.”
{1 Samweli 3:13.}

Eli alikuwa mtu mwema, mwadilifu; ila alikuwa mzembe katika malezi. Aliangukiwa na ghadhabu ya Mungu kwa vile hakuimarisha mambo madhaifu katika tabia yake. Hakutaka kuumiza hisia za mtu ye yote na hakuwa jasiri kukemea dhambi…

Alipenda usafi wa kitabia na haki; ila hakuwa na nguvu kimaadili kuweza kupinga uovu. Alipenda amani na umoja, hivyo akawa hamudu kukemea uovu na uhalifu. . .

Eli alikuwa mpole, mwungwana, anayejali huduma takatifu na mpenzi wa mafanikio ya kazi ya Mungu. Ni mtu aliyekuwa shujaa wa maombi. Kamwe hakuinuka kupingana na Neno la Mungu. Ila alikuwa na mapungufu, hakuwa jasiri kukemea dhambi na kutekeleza hukumu; hivyo akashindwa kutimiza jukumu la kusimamia taifa la Israeli lidumishe kweli na utakatifu. Katika imani yake, alishindwa kuongezea ujasiri na uthubutu wa kusema Hapana kwa wakati sahihi na mahali sahihi.

Eli alikuwa anajua mapenzi ya Mungu. Alijua ni tabia gani inampendeza Mungu, na ipi ni chukizo kwake. Hata hivyo aliwaachia watoto wake wakue na tamaa mbaya zisizotawalika, uchu usiojua kiasi, na maadili potofu.

Eli alikuwa amewafundisha watoto wake sheria ya Mungu, naye ameishi maisha yaliyo kielelezo chema; ila hapo bado alikuwa hajatimiza jukumu. Mungu alimhitaji yeye kama baba na kuhani, awazuie kufuata mapenzi yao maovu. Hilo alishindwa kufanya.

Wale wenye ujasiri kidogo mno kiasi cha kutothubutu kukemea uovu, au kwa sababu ya uzembe au kutokujali hawafanyi jitihada zo zote kuisafisha kiroho familia yao au kanisa la Mungu, watawajibika mbele za Mungu kwa uovu ulio matokeo ya upuuziaji wa majukumu yao. Tunawajibika kwa maovu ambayo yamewapata watu katika jamii kama matokeo ya sisi kama wazazi au wachungaji kushindwa kuyazuia yasitokee, kwa vile tulikuwa wazembe katika malezi ya watoto wetu.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: one or more people and outdoor
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.