“Tumemfanyia Bwana dhambi … Mlilie Bwana, Mungu wetu, kwa ajili yetu.” 1Samweli 7:6, 8.
Samwel alitembelea miji na vijiji katika nchi yote akijaribu kuwavuta watu mioyo yao imgeukie Mungu wa baba zao; na juhudi zake zilizaa matunda. Baada ya kunyanyaswa na adui zao kwa miaka ishirini, Israeli “walimlilia Mungu.” Samweli aliwashauri, “Ikiwa mnamrudia BWANA kwa mioyo yenu yote, basi iondoleeni mbali miungu migeni, nayo Maashtorethi yatoke kwenu, mkamtengenezee BWANA mioyo yenu, mkamtumikie yeye peke yake.” Hapa twaona uchaji Mungu halisi, dini ya moyoni ilifundishwa katika siku za Samweli kama Kristo alivyofundisha alipowasili hapa duniani. Pasipo neema ya Kristo, taratibu zote za kidini zilizokuwa zikifanyika, zilikuwa dini ya nje isiyo na manufaa yo yote ya kiroho kwa Israeli. Hata katika Israeli ya leo taratibu za kidini pasipo neema ya Kristo, hazifai kitu.
Lipo hitaji leo la uamsho wa dini ya kweli ya rohoni kama ilivyokuwa kwa Israeli ya zamani. Toba ndiyo hatua ya kwanza ipaswayo kuchukuliwa na wote wanaotaka kumrudia BWANA. Hakuna awezaye kutenda kazi hii kwa ajili ya mwingine. Tunapaswa kujinyenyekeza nafsi zetu mbele za Mungu na kuondolea mbali miungu yetu ya kigeni. Tunapokuwa tumetenda yote tuwezayo kutenda, BWANA atatufunulia wokovu wake. . . .
Mkutano mkubwa ulikuwa umekutanika kule Mispa. Hapa kulitangazwa wapate kufunga. Kwa kujidhili mbele za BWANA watu waliungama dhambi zao; na kama ishara ya nia yao ya dhati kutii maagizo waliyopatiwa, walimsimika Samweli kuwa mwamuzi . . .
Wakati Samweli akiwa kwenye zoezi la kumtoa mwanakondoo kama sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti waliwasili hapo jirani kwa vita. BWANA akapiga ngurumo, ukasikika mshindo mkubwa sana katika jeshi lililokuwa linawasogelea, wote wakafa ardhi ikajawa miili ya askari mashujaa. Wana wa Israeli walisimama wakishangaa, wakitetemeka kwa tumaini na hofu. Walivyoona adui zao walivyokatiwa mbali, walijua kuwa Mungu amekubali toba yao. . .
Kwa mataifa na kwa mtu binafsi, njia ya utii kwa Mungu ndiyo njia ya usalama na furaha, wakati njia ya uasi mwisho wake ni maafa na kushindwa.
Mungu akubariki unapofanya uamsho.....
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon