usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
Warumi 12:21.
Kristo mwenyewe, "aliposhindana na Ibilisi, na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kumshitaki kwa kumlaumu." Yuda 9. Kama angalifanya hivyo, angalijitia upande wa Shetani; kwani mashtaki na lawama ndizo silaha za yule mwovu. Katika Maandiko ameitwa jina lake "mshitaki wa ndugu zetu." Ufunuo 12:10.
Na Yesu asingalitumia silaha yoyote ya Shetani. Alisema tu, "Bwana na akukemee." Yuda 9.
Inatupasa kufuatisha mfano wake. Kama tumeingizwa ktk kushindana na adui za Kristo, Inatupasa tusiseme neno lolote la kurudisha ukali kwa ukali, ama neno linaloonekana kuwa ni neno la lawama. Yeye aliye mnenaji wa Mungu haimpasi kunena maneno ambayo Mfalme wa Mbinguni asingeyatumia ktk kushindana na Shetani. Yatupasa kumwachia - Mungu kazi ya kuhukumu na kutoa adhabu.

EmoticonEmoticon