NI HEKIMA KUBWA KUWANYAMAZIA WALE WANAOKUSEMA VIBAYA

MITHALI 26:4.

Usipende kujibu kila neno linalokushambulia wewe, wala usipende kujibu shutuma inayokushutumu wewe.

Usipende kujitetea sana ili kuonekana usie na hatia mbele za watu kwa kuwa wao huangalia nje na wala hawafahamu ukweli wa moyo wako.

Hata iweje huwezi kuwaridhisha wanadamu, ukiwajibu hili watauliza lile, kwa kuishi na kuwajibu kila wanalolianzisha utajikuta unakuwa mtumwa wa watu hao.

Kunyamaza ni silaha yenye sumu kali sana kwa watu wanaokushutumu uongo, mwisho wa siku hujiona wajinga kwa kumshutumu mtu hasiewajibu.

Tatizo kubwa la watu hupenda kusemwa vizuri na kusifiwa kila jambo wafanyalo, sio vibaya kusemwa vizuri ama kusifiwa lakini tambua ya kwamba huwezi kuwaridhisha wanadamu wote.

Jifunze kutenda yaliyo sahihi kwa Mungu wako na usisubiri maneno mazuri kusonga mbele.
Unaweza kutenda mema na ukaambulia lawama, matusi, kejeli na kashfa.

Hii ndiyo sababu unapaswa kujiepusha na kujibizana na watu bali tumia muda mwingi kufanya mambo yako ya msingi na kusonga mbele.

Hacha kujibizana na watu kaa kimya na Mungu atakupigania.

Mungu akupe kushinda kila neno baya linalosemwa kwa uongo juu yako.
Image may contain: 1 person, smiling, text

Previous
Next Post »
Powered by Blogger.