NINASIKIA SAUTI YA KONDOO



“Najuta, kwa sababu nimemtawaza Sauli awe mfalme; maana amerudi nyuma, asinifuate, wala hakufanya nilivyomwamuru.”
1 Samweli 15:11.

Wakati Sauli na jeshi lake wakipiga gwaride kuelekea nyumbani baada ya ushindi, kulikuwa na kilio kikuu nyumbani mwa Samweli nabii. Amepokea ujumbe kutoka kwa BWANA akikemea hatua aliyoichukua mfalme. Nabii alighadhabishwa sana mwenendo wa mfalme mwasi, akaomboleza na kuomba usiku mzima kusihi Mungu laiti angalighairi kutekeleza hukumu hiyo kali ya kutisha.

Kujuta kwa Mungu siyo sawa na kujuta kwa mwanadamu. “Tena Yeye aliye Nguvu za Israeli hatanena uongo, wala hataona majuto; maana siye mwanadamu, hata ajute.” Kughairi kwa mwanadamu huhusu badiliko la maamuzi akilini. Kughairi kwa Mungu humaanisha badiliko la mazingira na mahusiano. Mwanadamu anaweza kubadili mahusiano yake na Mungu kwa kutii masharti yatakayokidhi ukubali wa Mungu, ama, anaweza kwa utendaji wake binafsi, kujiweka nje ya upande mzuri ukubaliwao na BWANA; ila BWANA yeye ni yule yule “jana, leo, na hata milele” (Waebrania 13:8). Kutotii kwa Sauli kulibadili uhusiano wake na Mungu; ila masharti ya kupata ukubali wa Mungu hayabadiliki matakwa ya Mungu ni yale yale, kwani kwake “hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeuka-geuka.” (Yakobo 1:17).

Kwa moyo wa kuugua nabii aliamua kesho yake asubuhi aende kukutana na mfalme mwasi. Samweli alidumisha tumaini kwamba, kwa kutafakari, Sauli anaweza kutambua dhambi yake, na kwa toba na kujidhili apate kurejezwa tena kwenye uhusiano na Mungu. Ila hatua ya kwanza ielekezwapo katika kuasi, njia hufunguka kuendelea kuasi. Sauli akiwa amepofushwa na ukaidi wake, alikuja kukutana na Samweli akiwa na uongo midomoni mwake. Alitamka, “Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA.” Sauti zilizosikika masikioni mwa nabii zilipingana na kauli ya medal me kaidi.

Sauli alikana dhambi yake huku kelele za sauti za ng’ombe na kondoo zikiwa zinatangaza hatia yake.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

No automatic alt text available.
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.