“Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katikad kondoo walio wazuri, na ng’ombe na vinono, na wana-kondoo, na cho chote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza.”
1 Samweli 15:9.
Tangu anguko la Wafilisti pale Mikmashi, Sauli amefanya vita dhidi ya mataifa ya Moabu, wana wa Amoni, Edomu, Waamaleki na Wafilisti; na kila alipogeuka ili kupambana alipata ushindi mkuu. Alipopata agizo dhidi ya Waamaleki, kwa haraka alitangaza vita. Licha ya mamlaka yake kama mfalme alipata uungwaji mkono na nabii, hivyo alipotoa wito wa vita, wanaume wa Israeli walifurika kwake. Pambano dhidi ya Waamaleki halikupaswa kufanyika kwa sababu za kujinufaisha nafsi; Waisraeli hawakupaswa kupokea heshima za ushindi au kuteka nyara mali za adui zao. Walipaswa kuingia vitani kama tendo la utii kwa agizo la Mungu, kwa kusudi la kutekeleza hukumu dhidi ya Waamaleki. Mungu alikusudia mataifa yote yashuhudie hukumu kali dhidi ya taifa hilo ambalo limemkufuru Mungu, na itambulike kuwa waliangamizwa na watu wale wale waliowadharau . . .
Ushindi huu dhidi ya Waamaleki ulikuwa ushindi bora ambao Sauli alishawahi kujipatia, nao uliamsha kiburi moyoni, jambo ambalo lilikuwa hatari kwake. Agizo la kuwaangamiza kabisa hawa adui za Mungu lilitekelezwa, ila siyo kwa ukamilifu. Ili kujitafutia sifa na umashuhuri, Sauli aliamua kurudi na mfalme mateka, akiiga desturi za mataifa yanayowazunguka, mfalme katili na mwenye kupenda vita toka taifa la Amaleki. Watu wakajihifadhia wenyewe kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wanakondoo, kwa kisingizio kuwa ng’ombe hao wamehifadhiwa ili kutolewa kama sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. Ila kwa hakika kusudi lao halisi lilikuwa kutaifisha mifugo hiyo kwa manufaa yao binafsi.
Sauli sasa alikuwa amekabiliwa na mtihani wake wa mwisho. Upuuziaji wake wa mapenzi ya Mungu, akionesha kusudio lake la kutawala kama mtawala huru asiyewajibishwa na mwingine, alidhihirisha kuwa hawezi kutumainiwa kukabidhiwa mamlaka ya utawala kama mwakilishi wa BWANA.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon