Samweli akasema, Sitarudi pamoja nawe; kwa sababu umelikataa neno la BWANA, BWANA naye amekukataa wewe, usiwe mfalme wa Israeli.
1 Samweli 15:26.
Sauli alipoona kuwa Samweli amekoma kumletea ujumbe toka kwa Bwana, alijua kuwa Bwana alikuwa amemkataa kwa sababu ya njia yake ya uovu, na tabia yake ikaonekana nyakati zote kuvuka mipaka. Watumishi wake … nyakati zingine walishindwa kumkaribia, maana alionekana kama mtu aliyerukwa na akili, mkali na mkatili. Mara nyingi alionekana kujawa na majuto. Alikuwa mwenye uchungu, na mara kwa mara mwoga hata mahali pasipo na hatari … Muda wote alijawa na wasiwasi, na mara kwa mara akiwa katika hali ya msongo hakutaka usumbufu wowote, na nyakati zingine hakuruhusu yeyote kumwendea… Alirudia misemo ya kiunabii dhidi yake mwenyewe kwa unyonge, hata mbele za wasaidizi wake na mbele za watu.
Wale walioshuhudia Sauli akifanya vituko hivi vya ajabu walishauri asikilize muziki, kwa vile una uwezo wa kutuliza katika hali ya msongo. Kwa majaliwa ya Mungu, akajulishwa kwamba Daudi ni mwana muziki mahiri . . .
Upigaji kinubi wa Daudi kwa ustadi, ulituliza roho ya Sauli iliyokuwa imefadhaika sana. Kadiri alivyosikiliza muziki mzuri ukipigwa, ule mziki ulikuwa na nguvu ya kuondoa ule msongo mawazoni na kurejesha akili zake katika hali ya kawaida ya furaha.
Sauli aliondolewa nguvu zake, kwa sababu alishindwa kufanya amri za Mungu kuwa kanuni inayotawala maisha yake. Ni jambo la kutisha kwa mtu kupambanisha matakwa yake na yale ya Mungu, kama yalivyofunuliwa katika matakwa yake mahususi. Heshima yote ambayo mtu anaweza kuipata katika kiti cha enzi cha ufalme, itakuwa fidia duni kwa kukosa ukubali wa Mungu kupitia tendo la kutomtii. Kutotii amri za Mungu kunaweza tu kuleta majanga na kudhalilika hatimaye. Mungu amempatia kila mtu kazi yake kama vile alivyompa Sauli kusimamia serikali ya Israeli; fundisho yakini na muhimu hapa ni kwamba tutekeleze majukumu yetu kwa namna ambayo tutakutana na kumbukumbu za maisha yetu za utendaji kazi kwa furaha, na wala si kwa huzuni.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon