“BWANA akamwambia Samweli, Ijaze pembe yako mafuta, uende, nami nitakupeleka kwa Yese, Mbethlehemi; maana nimejipatia mfalme katika wanawe.”
1 Samweli 16:1.
Kafara ilipoisha, hata kabla ya kushiriki sherehe ya sadaka, Samweli akaanza utafutaji miongoni mwa wana wa Yese waliooneka waadilifu. Eliabu ndiye alikuwa mkubwa kuliko wote, umbo lake na uzuri wake vililandana na vile vya Sauli kuliko wale wengine wote. Utulivu wake na mwonekano mzuri wa umbo vilivuta macho na akili ya nabii. Samweli alipoona mwonekano wake wa kifalme, akawaza, “Kwa hakika huyu ndiye mtu ambaye Mungu amemchagua kuchukua nafasi ya Sauli.” Lakini Yehova hakuangalia mwonekano wa nje. Eliabu hakumcha Bwana. Kama angepewa kiti cha ufalme, angekuwa mfalme mkali na mwenye kiburi …
Hakuna uzuri wa nje uwezao kufanya mtu kukubalika mbele za Mungu. Hekima na umahiri unaodhihirishwa katika tabia na mwenendo, ndio huonesha uzuri wa kweli wa mtu; na ni thamani ya ndani, ubora wa juu wa moyo, vinavyofanya tukubalike mbele za Bwana wa Majeshi. Ni kwa ndani kiasi gani ukweli huu unaweza kuzama mioyoni mwetu hasa kuhusiana na namna tunavyotathmini hali yetu ya kiroho na ile ya wengine. Tunaweza kujifunza kutokana na kosa la Samweli jinsi isivyofaa tathmini inayolenga katika uzuri wa uso na mwonekano mzuri wa umbo._
Kaka wakubwa, ambao Samweli alitaka kuchagua mmojawao kuwa mfalme, hawakuwa na sifa ambazo Mungu aliziona kuwa za msingi kwa mtawala wa watu wake. Mwenye kiburi, mbinafsi, anayejitumainia, viliwekwa kando toka kwa yule ambaye hawakumdhania, yule aliyekuwa amedumisha usahili na uaminifu wa ujana wake, na ambaye ingawa mdogo machoni pake mwenyewe, angeweza kufunzwa na Mungu kubeba majukumu ya ufalme. Kwa hiyo leo, katika watoto wengi ambao wazazi wasingewadhania, Mungu anaona karama kubwa kuliko zile zionekanazo kwa wengine ambao wanadhaniwa kuwa watakuwa wa manufaa makubwa. Na kuhusiana na uwezekano maishani, ni nani awezaye kuamua kuwa kipi ni kikubwa na kipi ni kidogo? Ni wafanyakazi wangapi katika mazingira duni ya maisha, kwa kuanzisha njia za kubariki ulimwengu, wamepata mafanikio makubwa ambayo wafalme wanayaonea wivu!_
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon