KUJIANDAA KUONGOZA



“Daudi akamwambia Sauli, Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake, na alipokuwa akija simba, au dubu, akamkamata mwana-kondoo wa lile kundi, mimi hutoka nikamfuata, nikampiga, nikampokonya kinywani mwake; na akinirukia, humshika ndevu zake, nikampiga, nikamwua”
1 Samweli 17:34, 35.

Daudi aliendelea kukua akimpendeza Mungu na wanadamu. Alikuwa ameelekezwa kutembea katika njia ya Bwana, na sasa alidhamiria kufanya mapenzi ya Mungu kuliko hapo nyuma. Alikuwa na mada mpya za kutafakari. Alikuwa amekaa ikulu na kuona majukumu ya mfalme. Alikuwa amejua baadhi ya majaribu yaliyomseta Sauli na kujipenyeza katika tabia na utendaji wa mfalme huyu wa kwanza wa Israeli. Alikuwa ameona utukufu wa mfalme ukifunikwa na wingu zito la huzuni, na alijua kwamba kaya ya SauIl katika maisha yao ya kifamilia hawakuwa na furaha. Haya yote yalichangia kuifadhaisha roho ya huyu aliyekuwa ametiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli. Lakini wakati akiwa amezama katika kutafakari, na kusumbuliwa na fikra za hofu, akageukia kinubi chake, na kupiga muziki ambao ulielekeza fikra zake kwa mwanzilishi wa kila lililo jema, na wingu zito lililoonekana kutenda kufunika ukingo wa siku za usoni likaondolewa.

Mungu alikuwa akimfundisha Daudi masomo ya kumtumaini. Kama vile Musa alivyofunzwa kwa kazi yake, vivyo hivyo Bwana alikuwa akimwandaa mwana wa Yese kuwa kiongozi wa watu wake aliowachagua. Katika kuchunga kundi lake, alikuwa akijifunza juu ya uangalizi mkubwa zaidi ambao Mchungaji Mkuu anao kwa kondoo wa malisho yake.

Milima na mabonde ambamo Daudi alizunguka na mifugo yake, yalikuwa ni maficho ya wanyama wakali na wawindaji wa porini. Si mara chache simba toka vichaka vya Yordani au dubu toka milimani, walikuja, wakali wenye njaa, kushambulia kundi. Kwa desturi ya wakati ule Daudi alikuwa na silaha ya kombeo na fimbo ya mchungaji; na bado katika umri wake mdogo alithibitisha nguvu na ujasiri wake katika kulinda mifugo yake. . . .

Uzoefu wake katika mambo hayo uliimarisha moyo wa Daudi na kumjengea ujasiri na imani.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.