Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitilia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, ktk mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo na thamani kuu mbele za Mungu.
Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao.
1Petro 3:3-5.
Je Uliwahi kujiuliza kwann wanawake weengi wana mapepo??
Uliwahi kujiuliza kwa nn kina mama ndio waongozao kwa magonjwa meengi kuliko kina baba?!
Sikia nikwambie ndugu, shetani anafahamu saana namna ubongo wa mwanadamu unavyofanya kazi, amejifunza kwa muda wa miaka 6000, na aligundua kiumbe kilicho chepesi kukitumia ni mwanamke, maana anajua mwanaume kumuangusha ni ngumu sana ni mpaka kupitia kwa mwanamke!!!
Hivyo shetani alibuni mambo mbali mbali kupumbaza akili za kina Dada ili awaweke kwenye himaya yake kisha iwe rahisi pia kumpata mwanaume kama ilivyokuwa ktk bustani ya Edeni alivyomrubuni Mama yetu Hawa kisha akafanikiwa kumpata mwanaume Adamu!!!
"
"Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye. Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia ktk hali ya kukosa. Walakini ataokolewa kwa uzazi wake, kama wakidumu ktk imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi".
1Timotheo 2:13-15.
Shetani ndivyo afanyavyo leo yale aliyoyafanya busitanini Edeni ndivyo yanavyojirudia leo Hawa alidanganywa akaingia dhambini, Yesu akaja akatufundisha namna ya kumpinga Adui, alitufundisha kupitia neno lake twaweza kuyajua makusudi ya adui na kuyapiga hivyo tukaupata ushindi kwa imani tukimwangalia Mungu ktk Kristo Yesu!
Biblia imeandika "kujipamba kwenu kusiwe kwa kusuka nywele" fungu liko wazi, lakini leo utakuta kina dada wameshona mawigi, mitindo mbali mbali mingine mpaka inaitwa twende kilioni...
Utajiuliza kila mara hao waliosuka nywele utakuta wanalalamika kichwa kinawauma, wakati mwingine macho hayaoni vizuri, wengine walio ktk ndoa utasikia wanasema nikimaliza tendo la ndoa na mume wangu upata muwasho mkali sana sehemu za siri, wengine wanalalamika kusikia vitu vikiwatembelea mwilini.... Karibu ya hayo yoote hayo usababishwa na matumizi ya madawa ya nywele ama nywele za bandia, viwanda vyote vya nywele vipo chini ya shetani hivyo zile nywele unazosukia ama dawa utumiazo zinakuwa na nguvu za Giza ndani yake hivyo kukusababishia madhara makubwa mwilini, ikiwepo kufungwa akili usitambue mambo ya kiroho maana tayari umemkaribisha shetani kichwani mwako na kukutawala huku taratibu akienda kufunga akili ya mume wako kupitia muungano wenu wa ndoa, hivyo baada ya muda wote wawili mnakuwa mateka wa adui, kinachofuata mmomonyoko wa maadili unatokea!!!
Taratibu utajikuta unaanza kuvaa suruali, vipedo, na nguo chafu zisizompendeza Mungu, na kupitia wewe unakuwa mvuto mbaya kwa jamii na kuwasababisha wengine wafuate mtindo wako, wakati huo ukivaa suruali, "(Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako. Kumbukumbu 22:5)"
maana shetani anajua mwanaume ameumbwa kwa kutamani huvaapo suruali sehemu za siri ujichora hivyo unakuwa bango la shetani kuwaangusha wengi ktk dhambi ya uzinzi ama kwa kuvaa nguo fupi... Maana biblia inasema "(Mmesikia kwamba imenenwa, Usizini; lakini Mimi nawaambia, kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni wake. Mathayo 5:27,28.)"
Hivyo ndivyo shetani afanyavyo kazi yake kuu ya kuharubu akili za watu na kuzipeleka kwenye uharibifu, nywele ni moja ya vitu shetani avitumiavyo saana kupotosha ulimwengu vipo vingi avitumiavyo, kupitia wanawake japo wanaume pia kuna mitego yao lakini wanawake wamezidi funguka leo amua kumtafuta Mungu nawe utafanikiwa saana. Soma Biblia ikae kichwani shetani akujiapo mwambie "Imeandikwa"
Mtume Yakobo anatuambia "Basi mtiini Mungu, Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu naye atawakaribia ninyi, Itakaseni mikono yenu, enyi wenye nia mbili. Yakobo 4:7,8".
Dada zetu wanapaswa kuvaa kwa wepesi mavazi ya kawaida tu. Wanapaswa kuvaa mavazi ya kujisitiri, ya heshima na adabu pamoja na utulivu. Toa kwa ulimwengu kielelezo kilicho hai cha kujipamba kwa ndani kwa pambo la neema ya Mungu.- 3SM 242 (1897).
Mwonekano wa nje ni ishara kuonyesha jinsi moyo wa mtu ulivyo.- IT 136 (1856).

EmoticonEmoticon