MSAMAHA ULETA AMANI MOYONI.



masamaha au shukrani vinaweza kuwa dawa ya kuponya na ambayo hutuwezesha kukabiliana na maradhi ambayo hutokana na uhusiano wa kikatili. Kama mtu amekuudhi sana na ukashindwa kumsamehe, unamfanya akuumize mara ya pili. 

Roho ya kutosamehe huharibu afya na kutufunga ktk Uchungu. Hutupora furaha ambayo Mungu anataka tuwe nayo.
Kama Yesu alivyowasamehe wale waliokuwa wanamsulubisha wakati walikuwa hawastahili, ndivyo tunavyoweza kuwasamehe wale waliotujeruhi wakati hawastahili.

Kusamehe wengine haina maana tunakubaliana na matendo yao au tunahalalisha waliyotutendea. Badala yake, msamaha humtoa mtu mwingine ktk hukumu yako wakati hastahili, kwa kuwa Yesu alitutoa ktk hukumu yake wakati hatustahili. Kama mtume Paulo anavyosema, "tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi" (Waefeso 4:32)

Moja ya maswali ambayo watu huwa nayo wanapokutana na kihoro cha kuumiza moyo kinacholetwa na uhusiano wa kikatili, "Mungu anahusikanaje ktk jambo hili? Uchungu na kutokutendewa haki vimejaa ulimwenguni. Wakati mwingine maisha hayatendi haki tu.

Tunaishi ktk ulimwengu wa mema na mabaya, furaha na huzuni, upendo na chuki, afya na maradhi. Wakati mwingine tunajisababishia Uchungu sisi wenyewe kwa uamuzi wetu usiofaa, lakini mara nyingi tunakuwa hatujafanya jambo lolote baya lakini huzuni utunyemelea.
Lakini pamoja na maisha kukosa haki, Mungu bado yuko karibu. Naye hatatuacha (Ebr 13:5). Kinyume chake, tukimruhusu, atatutia nguvu na kutupatia ujasiri. Bado anaponya mioyo iliyovunjika, huwaweka huru wafungwa, na kuwaokoa wanaoonewa (Luka 4:18).

Image may contain: text, nature and outdoor
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.