“Hata ninyi nyote mkafanya fitina juu yangu, … wala hapana mmoja wenu anayenisikitikia.”
1 Samuel 22:8.
Roho ya uovu ilikuwa juu ya Sauli. Alijisikia kwamba adhabu yake haiepukiki kutokana na ujumbe wa onyo wa kukataliwa toka katika kiti cha ufalme wa Israel. Kule kuyaacha matakwa bayana ya Mungu sasa kulileta matokeo halisi. Hakugeuka, akatubu, akinyenyekeza moyo wake mbele za Mungu, bali aliufungua na kupokea kila ushauri wa adui. Alisikiliza kila ushuhuda wa uongo, akipokea kwa shauku kila kilichoweza kuchafua tabia ya Daudi, akitumaini kwamba anaweza kupata kisingizio kwa kuonesha bayana wivu wake ulioendelea kuongezeka na chuki kwa yule ambaye alikuwa amepakwa mafuta kukwea kiti cha enzi cha Israeli.
Kila uvumi ulikubaliwa kama kweli, haidhuru hauhusiani wala kuendana na jinsi tabia ya Daudi ilivyokuwa. Kila ushahidi kwamba ulinzi wa Mungu ulikuwa na Daudi ulionekana kumfanya mchungu zaidi na mwenye nia thabiti zaidi kumshughulikia Daudi. Kushindwa kutimiza mipango yake kulionekana kutofautiana sana na mafanikio ya mkimbizi huyu katika kukwepa mitego yake ya kunaswa, lakini hilo lilisaidia kufanya nia ya mfalme kuwa thabiti zaidi. Hakuwa mwangalifu vya kutosha kuficha mipango yake ya kumdhuru Daudi, wala mwangalifu juu ya mbinu za kutumia kutimiza makusudi yake.
Haikuwa Daudi mwanadamu, ambaye hakuwa amemkosea lolote, ambaye alikuwa anapambana naye. Alikuwa katika mapambano na mfalme wa mbinguni; Kwani Shetani akiruhusiwa kutawala moyo ambao hauko chini ya uongozi wa Yehova, atauelekeza sawasawa na mapenzi yake, mpaka mtu huyo aliye chini ya mamlaka yake awe wakala mfanisi katika kutimiza mipango ya Shetani. Kwa hiyo uadui wa mwanzilishi wa dhambi kwa makusudi ya Mungu ni mkali sana, uwezo wake wa kutenda maovu ni wa kutisha kiasi kwamba watu wanapojitenga na Mungu, mvuto wa shetani huwa juu yao, na akili zao zinaendelea kutiishwa, mpaka wanapoteza kabisa kicho cha Mungu, na heshima kwa wanadamu, na kuwa maadui wa Mungu na watu wake, wajasiri na waliopania. Mungu anachukia dhambi yote, na mtu kwa kurudia rudia anapokataa mashauri yote ya mbingu anaachwa kuwa chini ya udanganyifu wa Shetani.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon