“Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.”
1 Samweli 17:45.
Goliathi akaharakisha kumwendea Daudi na kumlaani kwa miungu yake. Aliona kuwa kwa heshima yake, lilikuwa tusi kuletewa kijana mdogo tu, bila silaha za kivita, kuja kukabiliana naye… Daudi hakuudhika maana hata hivyo walimdhania kuwa yeye ndiye aliyekuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa, hivyo hakutetemeshwa na vitisho vyake, bali alijibu: “Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.” Hotuba hiyo, ikitolewa kwa sauti inayosikika vyema, tena ya kimuziki, ilisikika angani, na bila shaka ilisikika vyema kwa maelfu waliokuwa wamekusanyika kwa vita. Hasira ya Goliathi ilipanda kufikia upeo. Kwa hasira akafunua chepeo iliyokuwa ikikinga uso wake na kuharakisha ili akamwadhibu mpinzani wake. Mwana wa Yese alikuwa tayari kukabiliana na adui yake. “Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti. Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.”
Majeshi ya pande zote mbili yakapigwa butwaa. Walikuwa wameamini kwamba Daudi angeuawa; lakini jiwe lilipoenda likipuliza angani, mpaka kwa lengo lake, na kupenya ndani, walimwona shujaa wa kutisha akipepesuka na kutapatapa kama aliyepigwa na upofu. Lile jitu likayumbayumba na kupepesuka na kama mwaloni uliopigwa akaanguka chini. Daudi hakupoteza muda. Alikimbia kumwelekea Mfilisti huyu aliyeanguka chini, na kwa mikono miwili akachomoa upanga wa Goliathi. Muda mfupi kabla ya hapo Goliathi alikuwa ametamba kwamba kwa upanga huu atakata kichwa cha kijana Daudi na kuacha mwili wake ukiliwa na ndege wa angani. Sasa upanga huu umeinuliwa hewani na kisha kichwa cha huyu mwenye kujigamba kikaviringika toka katika mwili wake, na sauti ya kushangilia ushindi ikapaa toka katika kambi ya Israeli.
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon