Daudi akasema, BWANA aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na BWANA atakuwa pamoja nawe.
1 Samweli 17:37.
Daudi alipoona kuwa Israel yote imejawa hofu, na kujua kuwa yule mfilisti amekuwa akifanya dharau ya namna hiyo siku hata siku, bila kupata shujaa wa kumnyamazisha, roho yake ikawaka ndani yake. Akajawa shauku ya kulinda heshima ya Mungu aliye hai na sifa za watu wake.
Daudi, katika unyenyekevu wake na bidii kwa ajili ya Mungu na watu wake, akaomba apambane na huyu mwenye kujigamba. Sauli akakubali na Daudi akavalishwa mavazi na kupewa silaha za Sauli. Akavua silaha na mavazi ya mfalme maana alikuwa hajawahi kuyajaribu. Alikuwa amemjaribu Mungu, na kwa kumtumainia alikuwa amepata ushindi maalumu mara nyingi. Kuvaa mavazi ya Sauli kungeashiria kwamba Daudi alikuwa shujaa wa kivita, wakati ambapo alikuwa mtoto Daudi aliyechunga kondoo. Hakutaka sifa yoyote iende kwa silaha za Sauli kwani tumaini lake lote lilikuwa kwa Bwana, Mungu wa Israeli.
Akachagua mawe matano laini toka katika kijito, akayaweka mfukoni na akiwa na kombeo lake mkononi mwake akamsogelea Mfilisti. Lile jitu likamkimbilia kwa jeuri, akitaraji kukutana na jitu lenye nguvu miongoni mwa mashujaa wa Israeli. Mbeba silaha wake akamtangulia na aliona kama hakuna ambacho kingesimama mbele zake. Alipomkaribia Daudi hakuona kitu isipokuwa kijana, akiitwa mvulana kwa vile alikuwa kijana mdogo. Sura ya Daudi ilikuwa nyekundu yenye afya, na umbo lake mwanana, akiwa hana silaha ya kumkinga, ilionekana kuwa fursa kwake, lakini kati ya mwonekano wake wa ujana na jitu kubwa shujaa la kifilisti, kulikuwa na tofauti ya kutisha.
Goliathi alipata mshangao na hasira. “Je mimi ni mbwa,” alisema Goliathi, “hata umenijia kwa fimbo?” Kisha akammiminia Daudi laana kwa miungu yake yote aliyoifahamu. Akapiga kelele kwa dharau, “Njoo huku kwangu; nyama yako nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni.”
”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

EmoticonEmoticon