MAJIVUNO YA MWANADAMU



Yule Mfilisti akasema, Nayatukana leo majeshi ya Israeli; nipeni mtu tupigane.
1 Samweli 17:10.

Vita ilipotangazwa kati Israeli na Wafilisti, vijana watatu kati ya wana wa Yese walijiunga na jeshi chini ya Sauli; bali Daudi alisalia nyumbani. Baada ya muda, hata hivyo, alienda kutembelea kambi ya Sauli. Kwa maelekezo ya baba yake alipaswa kubeba ujumbe na zawadi kuwapelekea kaka zake na kujua kama wanaendelea salama… Daudi alipokaribia kambi ya jeshi, alisikia sauti ya vurugu, kama vile walikaribia kuanza kupigana . . .

Goliath, shujaaa wa Wafilisti, alijitokeza, na kwa kutumia lugha ya matusi aliwadharau Israeli na kuwataka wachague mtu toka miongoni mwao ambaye ataenda kupambana naye. . . .

Kwa siku arobaini majeshi ya Israeli yalikuwa yakitetemeka mbele ya changamoto ya kiburi ya huyu shujaa wa kifilisti. Mioyo yao ilizimia walipolitazama hili jitu kubwa lenye urefu wa mikono sita na shubiri moja. Alikuwa na chapeo ya shaba kichwani, tena amevaa darii ya shaba; na uzani wake ile darii ya shaba ulikuwa shekeli elfu tano za shaba, tena amevaa mabamba ya shaba miguuni mwake. Vazi lake lilitengenezwa kwa mabamba ya shaba yakilazwa kila moja juu ya jingine kama magamba ya samaki, na yalikuwa yamesukwa kwa namna ambayo hakuna mshale ambao ungeweza kuyapenya. Katika mabega yake alibeba mkuki mkubwa ambao pia ulitengenezwa kwa shaba.” Na mti wa fumo lake ulikuwa kama mti wa mfumaji; na kichwa cha mkuki wake kilikuwa shekeli mia sita za chuma uzito wake; na mtu aliyemchukulia ngao yake akamtangulia.”

Israeli hawakumchokoza Goliathi, bali Goliathi alionesha majivuno na jeuri dhidi ya Mungu na watu wake Israeli. Dharau na majivuno na tambo zitatoka kwa yule mpinga kweli, ambao wanajifanya Goliathi. Lakini isionekane yoyote ya tabia hizi miongoni mwa wale ambao Mungu amewatuma kupeleka ujumbe wa mwisho wa onyo kwa ulimwengu ambao unaelekea kuangamia.

Goliathi alitumainia silaha zake. Aliyatisha majeshi ya Israeli kwa maneno yake ya majivuno, na dharau wakati akifanya onesho la kutisha la silaha zake, ambazo ndizo zilikuwa nguvu zake.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.