KUPIMWA NA KUONEKANA KUPUNGUA



“Hata mara alipokwisha kuitoa hiyo sadaka ya kuteketezwa, kumbe! Samweli akatokea. Naye Sauli akatoka kwenda kumlaki na kumsalimu.”
1 Samweli 13:10.

Mungu alielekeza wale tu waliowekewa mikono kuhudumu katika ofisi ya ukuhani ndio tu wahudumu mbele zake. Ila Sauli aliagiza, “Nileteeni hapa sadaka ya kuteketezwa;” huku akingali amevalia mavazi yake ya vita, akaikaribia madhabahu na kutoa sadaka mbele za BWANA. Iwapo Sauli angalizingatia masharti ya utii ambayo yangeruhusu msaada wa Mungu uambatane naye, angalishuhudia BWANA akitenda ukombozi mkuu kwa ajili ya Israeli, kwa kuwatumia wachache walio watiifu kwa mfalme. Ila Sauli alijiamini mwenyewe na utendaji wake kiasi kwamba alienda kumlaki nabii kama mtu astahiliye pongezi badala ya kuwa mtu astahiliye karipio. Sauli alianza kutetea mwenendo wake, na kumlaumu nabii; badala ya kujilaumu yeye binafsi. Wapo wengi wanaofuata njia hiyo. Kama Sauli wamepofuka na kuzama katika makosa yao. BWANA anapotafuta kuwarekebisha, hupokea maonyo kama kejeli, na kumkosoa yeye awaleteaye ujumbe wa kimbingu.

Iwapo Sauli angalikuwa mwepesi kuona kosa lake na kuliungama, uzoefu huu mchungu ungalikuwa fundisho kumfanikisha awe na tahadhari siku za usoni. Angeweza baada ya hapo kuepuka kufanya makosa yenye kusababisha ghadhabu toka kwa BWANA. Ila kwa kuona kwake kuwa anahukumiwa pasipo kosa, ni hakika ulikuwepo mwelekeo kuwa atarudia tena kutenda dhambi hiyo.

BWANA angependa watu wake, katika kila hali, wadhihirishe tumaini la dhati kwake. Japo hatuwezi kuelewa kikamilifu utendaji wa maongozi ya Mungu, yatupasa kusubiri kwa uvumilivu na unyenyekevu hadi ufike muda mwafaka atakapoona yafaa kutufunulia nuru husika.

Uasi wa Sauli ulidhihirisha kuwa hastahili kukabidhiwa jukumu kubwa takatifu. Kwa ustahimilivu angevumilia mtihani huo wa kiroho, ufalme ungethibitishwa kwake na kwa nyumba yake. Kwa hakika, Samweli amewasili hapo Gilgali kutekeleza kusudi hilo maalumu. Ila Sauli amepimwa katika mizani, na kuonekana amepungua. Sharti aondolewe katika madaraka yake ili kupisha mtu ambaye atamheshimu Mungu kupitia heshima na mamlaka aliyokabidhiwa.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.