KUMTANGULIA MUNGU



“Akangoja siku saba, kwa kadri ya muhula uliowekwa na Samweli, lakini Samweli hakuja Gilgali, na hao watu wakatawanyika mbali naye.” 1 Samweli 13:8.

Ilikuwa hadi mwaka wa pili wa kutawala kwake Sauli ambapo jitihada zilifanyika kuangamiza Wafilisti. Shambulio kali la kwanza lilifanywa na Yonathani, mwana wa mfalme, ambaye alishambulia na kuteka ngome yao iliyoko Geba. Wafilisti, wakiaibika kwa kushindwa huku, walijiandaa ili kuharakisha kupambana na Israeli. Sauli sasa alitangaza vita. . . .

Kabla muda ulioahidiwa na nabii haujapita, Sauli alikoswa uvumilivu kwa uchelewaji huo na kuruhusu akatishwe tamaa na hali iliyokuwa ikijitokeza mahali hapo . . .

Muda wa kumthibitisha Sauli umewasili. Kwa sasa alipaswa kuonesha endapo atamtumainia Mungu na kusubiri kulingana na agizo lake, hivyo kudhihirisha kwamba ni mtu ambaye Mungu anaweza kumtumainia katika nyakati za hatari kama mtawala juu ya watu wake, au kwamba atayumba na kuonesha kutostahili kubeba majukumu matakatifu aliyokabidhiwa.

Kwa kumchelewesha Samweli, lilikuwa ni kusudi la Mungu kwamba tabia ya moyo ya Sauli ipate kudhihirika, kwamba wengine wapate kujua ni nini angalilitenda wakati wa hatari. Ni jukumu ambalo hapaswi kulibeba, ila Sauli hakutii maagizo. Aliona haileti tofauti nani anawasiliana na Mungu, au kwa namna gani; hivyo kwa nguvu na kujiamini, alisonga mbele kutenda jukumu la kikuhani.

BWANA anao mawakala wake aliowateua kwa kila jukumu, na iwapo hao hawatambuliwi na kuheshimiwa na wale wanaohusiana na kazi yake, iwapo watu hujisikia huru kupuuzia maagizo yake, hawapaswi kubakizwa kwenye majukumu ya uongozi wa kazi ya BWANA. Hawazingatii ushauri, wala maagizo ya Mungu kupitia wakala wake aliowaweka. Kama Sauli, wataharakisha kutenda jukumu ambalo hawakuteuliwa kulihudumu, na makosa watakayoyatenda kwa kufuata matashi yao ya kibinadamu kutafanya taifa la Israeli la Mungu liingie kwenye hali ambayo itakwamisha Kiongozi wao asiweze kujifunua miongoni mwa watu wake.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.