HAKUNA UDHURU



“BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake ni shahidi leo, ya kuwa hamkuona kitu mkononi mwangu.”
1 Samweli 12:5.

Tamaa ya madaraka na fahari ni ngumu kuiponya leo kama ilivyokuwa zama za Samweli. Wakristo hutaka kujenga kama watu wa dunia wajengavyo; kuvaa kama watu wa dunia wavaavyo---kuiga desturi na mienendo ya wale ambao ibada yao huielekeza tu kwa mungu wa dunia hii. Mafundisho ya neno la Mungu, ushauri na maonyo kutoka kwa watumishi wake, na hata tahadhari zitumwazo moja kwa moja kutoka kiti chake cha enzi, huonekana hazina nguvu kuzikomesha tamaa hizi mbaya zisizofaa. Wakati moyo ukijitenga mbali na Mungu, kila udhuru huwa hoja kuhalalisha kupinga mamlaka ya Mungu . . .

Watu walio baraka mara nyingi hawathaminiwi. Wale waliotenda kazi kwa bidii na kwa kujitoa kwa ajili ya wengine, na ambao wametumika kufanikisha matokeo makuu, mara nyingi wamelipwa kejeli na upuuziwaji. Watu hao wanapoona kuwa wametupwa kapuni, ushauri wao kutozingatiwa au kubezwa, wanaweza kufikiri kuwa wanapitia uonevu mkuu. Ila hebu wajifunze kutoka kwa kielelezo cha Samweli wasijihesabie haki wenyewe, hadi pale Roho wa Mungu atakapoongoza kwa hatua kama hiyo.

Heshima anayopewa yeye anayehitimisha kazi ni bora kuliko shangwe na hongera za wale wanaoanza majukumu yao, ambao bado hawajajaribiwa.

Ni wangapi wanaostaafu katika nyadhifa za majukumu makubwa kama vile majaji/mahakimu, wanaoweza kutamka kuhusu usafi wao wa kuwa, “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye kuwa nina dhambi? Ni nani miongoni mwenu anayeweza kuthibitisha kuwa nimepindisha haki nikapokea rushwa? Kamwe sijawa na doa kama mwanadamu ila nimedumu kutenda haki na kweli. Nani anaweza kutamka kama Samweli ambaye alikuwa akiwaaga watu wa Israeli, kwa vile wamekusudia kuwa na mfalme? . . . Mwamuzi mwadilifu, jasiri! Ila ni jambo la kusikitisha mno kwamba mtu mwadilifu jinsi hiyo alilazimika kujinyenyekeza ili kutoa utetezi wake.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.