CHAGUO LA WATU



“Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka” 
1 Samweli 12:13.

Katika Sauli, Mungu aliwapatia Israeli mfalme waliyemtaka . . . Mwenye umbo zuri la madaha, mrefu wa kuvutia, mwonekano wake ukikubalika kwa matarajio yao kwa mfalme, na ujuzi wake na ujasiri kuongoza vita vilikuwa vyenye mvuto ulioibua heshima na hofu toka mataifa mengine. Hawakutilia mashaka yo yote kuwa mfalme wao anaweza kupungukiwa sifa zimwezeshazo kutawala kwa haki na usawa. Hawakutaka ambaye ana msingi wa tabia njema, mwenye kumpenda na kumcha Mungu. Hawakutafuta ushauri kutoka kwa Mungu kuhusu sifa zimpasazo mfalme, ili kudumisha hadhi yao kama taifa teule la Mungu. Hawakutafuta njia ya Mungu, wametafuta njia yao wenyewe. Hivyo Mungu aliwapatia mfalme waliyemtaka—mtu ambaye tabia yake ilifanana nao. Mioyo yao haikunyenyekezwa kwa Mungu, na mfalme wao alikuwa hajaruhusu nafsi yake kutawaliwa na neema ya Mungu. Chini ya utawala wa mfalme huyu watapata uzoefu utakaowawezesha kutambua kosa lao, wapate kumrudia BWANA.

Hata hivyo, baada ya BWANA kumkabidhi Sauli majukumu ya kuongoza ufalme, hakumwacha peke yake. Aliruhusu Roho Mtakatifu akae ndani yake amfunulie udhaifu wake na hitaji lake la neema ya Mungu; na Sauli endapo angemtumainia Mungu, BWANA angalikuwa naye. Kwa kadiri ambavyo mapenzi yake yangaliongozwa na mapenzi ya Mungu; kwa kadiri ambavyo angejisalimisha katika uongozi wa Roho wake, Mungu angeliheshimu bidii zake kwa kumpa mafanikio. Lakini Sauli alipochagua kufanya peke yake pasipo kumshirikisha Mungu, hapo ndipo Bwana alipokoma kuwa kiongozi wake, hivyo akalazimika kumwondoa kutoka kwenye wadhifa huo. Kisha BWANA akamwita na kumweka katika kiti cha enzi “mtu aupendezaye moyo wake” (1 Samweli 13:14)—siyo mtu ambaye hana kasoro kitabia, ila mmoja ambaye, badala ya kujitumainia nafsi, atamtegemea Mungu, na kuongozwa na Roho Mtakatifu; ambaye, anapotenda dhambi, atanyenyekea kukubali maonyo na marudi.

”Rehema za Bwana ni mpya kila siku asubuhi.”
(Maombolezo 3:22, 23).

Image may contain: 1 person, text
Previous
Next Post »
Powered by Blogger.