Msidanganyike. Mungu hadhihakiwi. Utakatifu tu, Wala si kitu kingine ndio utakaowafanya kuwa tayari kwenda mbinguni. Unyofu na uchaji wa hakika ktk mambo ya maisha peke yake ndio uwezo wa kuwapa tabia Safi, bora, na kuwawezesha kuingia mbele za Mungu akaaye penye nuru isiyoweza kukaribiwa.
Tabia ya mbinguni haina budi kupatikana hapa duniani, ama sivyo kamwe haipatikani tena. Basi anza mara moja. Usidanganyike kuwa utafika wakati uwezapo kujitahidi kwa urahisi kuliko sasa, kila siku uzidisha umbali wako kutoka kwa Mungu. Jitayarishe kwa ajili ya uzima wa milele. Zoeza mawazo ya moyo wako kuipenda Biblia, kuupenda mkutano wa maombi, kupenda saa kumtafakari Mungu, na zaidi ya yote saa ambayo Roho ushirikiana na Mungu. Uwe ni mwenye kufikiri mambo ya mbinguni ukipenda kuungana na lile kundi la waimbaji wa Mbinguni ktk makao ya juu.

EmoticonEmoticon