Yohana aliitwa kutazama kundi la watu walio tofauti na wale wanaomwabudu mnyama au sanamu yake kwa kutunza siku ya kwanza ya juma. Utunzaji wa siku hii ndiyo chapa ya mnyama - TM 133 (1898).
Chapa ya mnyama ni sabato ya kipapa. - Ev 234 (1899).
Wakati wa kupimwa utakapofika, maana ya chapa ya mnyama itaoneshwa dhahiri. Ni utunzaji wa Jumapili. - 7BC 980 (1900).
Ishara, au mhuri, wa Mungu unafunuliwa ktk utunzaji wa Sabato ya siku ya saba, ukumbusho wa Bwana wa uumbaji
........ Chapa ya mnyama ni kinyume cha huu - ushikaji wa siku ya kwanza ya juma - 8T 117 (1904).
"Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, .... Watiwe chapa ktk mkono wa kuume, au ktk vipaji vya nyuso zao" (Ufunuo 13:16). Siyo tu kwamba watu hawatafanya kazi kwa mikono yao siku ya Jumapili, bali pia kwa akili zao hawana budi kukiri kuwa Jumapili ni Sabato. - Special Testimony to Battle Creek Church (Ph 86) 6, 7 (1897).

EmoticonEmoticon